Mlima wa Huangshan
中国国际广播电台

      Kuna usemi wa Kichina usemao, “Ukitembelea Mlima wa Huangshan, haina haja kuangalia milima mingine ya China”. Usemi huu unamaanisha kuwa mandhari ya Mlima wa Huangshan ni nzuri zaidi kuliko milima mingine.

Mlima wa Huangshan uko kusini mwa China, mandhari ya mlima huo ni kilomita za mraba 1200, mlima mrefu, magenge makubwa, hali ya hewa inabadilika jinsi urefu unavyoongezeka kutoka chini, na kuna ukungu na mvua nyingi.

Mlima wa Huangshan una mandhari zake ambazo hazipatikani katika milima mingine, moja ni miti misonobari, miti hiyo yenye miaka zaidi ya mia moja iko zaidi ya elfu kumi, na mingi inakua kwenye nyufa za majabali; pili ni majabali yenye maumbo ya ajabu; tatu ni mawingu meupe yanayoelea katikati ya mlima; nne ni chemchemi ya maji ya moto.

Kutokana na hali ya hewa tofauti aina za mimea pi ni nyingi. Majani ya chai katika mlima huo ni maafuru sana nchini na nchi za nje.

Licha ya mandhari nzuri ya maumbile pia kuna utamaduni mkubwa kwenye mlima wa Huangshan. Washairi, wachoraji wa China ya kale waliwahi kutembelea huko na wameandika mashairi mengi ya kuusifu mlima huo.

Kutokana na mandhari nzuri ya mlima huo walitokea wachoraji wengi, na wapiga picha wa kisasa wanautumia mlima huo kama ni chimbuko la picha zao.

Mwaka 1990 UNESCO iliuorodhesha mlima huo katika urithi wa dunia.