www
Kinanda cha Liuqin
中国国际广播电台

     Liuqin inafanana na Pipa , inatengenezwa kwa mbao, ni kinanda kinachotutumiwa sana na watu wa mikoa ya Shandong, Anhui na Jiangsu, na kinatumika zaidi katika opera ya kienyeji.

Kinanda hicho kinatoa sauti kwa kukwaruzwa na vidole, mpiga anakiweka kifuani na kushika kinanda kwa mkono wa kushoto na kupiga kwa mkono wa kulia.

Mwishoni mwa 1958 mafundi wa kiwanda cha kutengenezea kinanda hicho waliongeza nyuzi za kinanda hicho kutoka mbili hadi tatu, sauti zikawa zimeongezeka. Katika miaka ya 70 kinanda hicho kimeongezwa nyuzi na kufikia nne. Kinanda hicho kimekuwa na historia ya miaka 200 nchini China.

Hivi leo kinanda hicho kimekuwa ala muhimu katika vikundi vya muziki wa Kichina, sauti yake ni kama Mandolin, na kikichanganywa na ala za muziki za Kimagharibi muziki unapata utamu mahsusi.

mnasikiliza: Maua Kapok yachanua