Kinanda Konghou
中国国际广播电台

      Kinanda Konghou kimekuwepo kwa miaka zaidi ya elfu mbili. Katika Enzi ya Tang (618-907), kutokana na ustawi wa uchumi, ala hiyo pia ilienea sana na hata ilijulishwa nchini Japan na Korea. Lakini katika karne ya 14 ala hiyo ilikuwa haitumiki sana na hatimaye ilitoweka, na ilionekana tu kwenye picha.

Kwa kufanya utafiti, wanamuziki wa China walifanikiwa kutengeneza ala hiyo katika miaka ya 80 ya karne iliyopita.

Kinanda hicho kina nyuzi 36 ziko juu ya boksi la kukuza sauti.

Eneo la sauti ya kinanda hicho ni kubwa, mpigaji anapiga kinanda hicho kwa mikono miwili.

Mnasikiliza:Mwanzi wa Hunan