Kinanda Erhu
中国国际广播电台

      Kinanda Erhu ni ala muhimu ya muziki wa Kichina, kilianza kutokea katika karne ya saba hadi kumi Enzi ya Tang. Katika miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, kinanda hicho kilikuwa kinatumika katika muziki wa opera.

Kinanda Erhu kina urefu wa sentimita 80, na kina nyuzi mbili, na kwenye sehemu ya chini kuna boksi la kukuza sauti kama kikombe, kinatoa sauti kwa upinde. Mpigaji anakaa na kuvuta upinde, baadhi ya watu wanakiita kinanda hicho kuwa ni “fidla ya Kichina”.

Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, kinanda hicho kiliwahi kufanyiwa mageuzi mara nyingi. Hiki ni kinanda ambacho kinaweza kuchezwa peke yake, lakini kinatumika zaidi kwa kushirikiana na ala nyingine katika muziki wa Kichina.

Erhu ni ala ya muziki iliyoenea sana miongoni mwa Wachina kutokana na sauti yake tamu.

Mnasikiliza : Milio ya ndege milimani