Xiao
中国国际广播电台

     Xiao ni ala nyingine inayotoa sauti kwa kupuliza. Ala hiyo ilipatikana zamani sana nchini China, na tokea mwanzo ala hiyo ilikuwa na jina hilo hilo. Kwenye paipu kuna vitundu na kwa kuziba vitundu hivyo kubadilisha sauti.

Mwanzoni Xiao ilitokea katika mikoa ya Sichuan na Gansu, na katika karne ya kwanza ala hiyo ilianza kuenea katika sehemu ya kaskazini.

Xiao inafanana sana na filimbi, lakini ni ndefu kuliko filimbi. Ala hiyo inatengenezwa kwa mwanzi, na kuna vitundu tano, vitundu vinne viko mbele na kimoja kiko nyuma, na kwenye sehemu ya mwisho kuna vitundu vitatu au vinne ambavyo vinasaidia kufanya sauti itoke zaidi.

Xiao inafaa kueleza hisia za upendo au za huzuni kutokana na sauti yake laini na nene, kwa hiyo mara nyingi hupigwa peke yake, lakini vile vile inatumika katika muziki wa Ki-guangdong na muziki wa opera kwa kushirikiana na ala nyingine.

Kuna aina nyingi za Xiao kutokana na urefu na unene tofauti.

Muziki maarufu “Bata buniki Wanaoelea Angani” unaeleza vizuri jinsi ndege walivyozunguka pole pole angani.

Mnasikiliza:Bata buniki wanaoelea angani