Guanzi
中国国际广播电台

      Guanzi ni aina nyingine ya paipu. Ala hiyo ilianza katika Enzi ya Han Magharibi miaka elfu mbili iliyopita mkoani Xinjiang nchini China, na baadaye ilienea katika sehemu ya kaskazini ya China.

Sauti ya Guanzi ni kubwa, ni ala ya muziki isiyoweza kukosekana katika muziki wa kienyeji wa sehemu ya kaskazini ya China. Ala hiyo inaweza kutoa sauti za aina mbalimbali hata kuiga milio ya wanyama.

Guanzi inagawanyika katika aina tofauti kutokana na ukubwa tofauti.

Muziki maarufu wa Guanzi peke yake “Mlango Mdogo” unapendwa sana na wasikilizaji kutokana na muziki wenyewe unavyoonesha jinsi watu wanavyofurahi.

Mnasikiliza: Xiaokaimen