Qing
中国国际广播电台

      Qing ina historia ndefu sana katika ala za muziki za kale, ni ala ya mawe na inatoa sauti kwa kugongwa.

Qing ilitumika sana katika zama za kale kwa ajili ya tambiko.

Kuna aina mbili za Qing, moja ni jiwe moja, nyingine ni mawe kadhaa. Qing ya jiwe moja inagongwa kwa ajili ya wafalme wanapofanya tambiko, na Qing yenye mawe mengi ni kwa ajili ya muziki katika kasri la kifalme.

Mwezi Agosti, mwaka 1978, kwenye kaburi la kale mkoani Hubei wataalamu wa mambo ya kale waligundua Qing, kengele mfululizo za muziki ambazo zimekuwa na miaka 2400. Jumla ya vipande 32 vya mawe ya Qing viligunduliwa. mwaka 1980 taasisi ya fizikia ya mkoa wa Hubei ilitengeneza vipande vya Qing kwa kuiga vya kale, sauti yake ilikuwa nzuri sana.

Mwaka 1983 kikundi cha nyimbo na dansi kilifanikiwa kutengeneza seti moja ya Qing yenye vipande vya mawe 32 ambayo inaweza kupiga muziki unaovutia sana.

Mnasikiliza:Matawi ya mianzi