Mtungaji Muziki Liu Wenjin
中国国际广播电台

Bw. Liu Wenjin ni mtunzi wa muziki mashuhuri nchini, alihitimu masomo yake mwaka 1961 katika chuo cha muziki cha taifa. Aliwahi kuteuliwa kuwa kiongozi wa bendi ya taifa ya ala za muziki za jadi, msimamizi mkuu wa sanaa na mkuu wa kundi la michezo ya opera ya taifa; hivi sasa yeye ni mwongozaji wa sanaa wa kundi la michezo ya opera la taifa. Mwaka 2001 aliajiriwa kuwa profesa wa chuo kikuu cha ala za muziki za jadi cha Korea ya Kusini.

Bw. Liu Wenjin alikuwa na mafanikio mazuri aliposoma chuoni na aliwahi kupata tuzo ya “mwanafunzi hodari” iliyotolewa na chuo cha muziki cha taifa. Alitunga muziki mwingi, na ule aliotunga mwaka 1999 “Ukuta Mkuu” ulipata tuzo ya ngazi ya kwanza ya taifa.

Katika miaka zaidi ya 40 iliyopita Bw. Liu Wenjin alitunga na kurekebisha muziki na nyimbo nyingi za kijadi, na kutunga muziki kwa ajili michezo ya ngoma, opera, sinema na michezo ya televisheni. Bw. Liu Wenjin pia alishiriki kwenye utungaji wa mchezo mkubwa wa nyimbo na ngoma ijulikanayo kwa “Nyimbo za mapinduzi ya China”.

Bw. Liu Wenjin amesifiwa na wanamuziki wa China kuwa ni mtunzi hodari wa muziki nchini China, mwezi Septemba mwaka 1989 bendi ya ala za muziki za jadi ya Hong Kong ilifanya maonesho ya muziki yajulikanayo kwa jina la “Toka Liu Tianhua hadi Liu Wenjin”.

Taasisi ya utafiti wa muziki wa China ya Amerika ya kaskazini ijulikanayo kwa “CHINESE MUSIC” inamsifu Liu Wenjin kuwa ni mwanamuziki mkubwa wa China bara, na kuchapisha makala nyingi za maelezo kuhusu muziki wa jadi aliotunga.

Bw. Liu Wenjin alialikwa kutembelea nchi makumi kadhaa zikiwemo za Ulaya, Marekani na Asia pamoja na sehemu za Hong Kong, Macao na Taiwan za China. Yeye na wanamuziki wa Japan na Korea ya Kusini walianzisha bendi ya muziki ya Asia.

Bw. Liu Wenjin aliteuliwa na wizara ya utamaduni kuwa msanii mwenye mafanikio makubwa, alitunukiwa shahada ya heshima na kupewa kiinua mgongo maalumu na serikali.   [Burudani za Muziki]Ukuta Mkuu