Gao Weijie
中国国际广播电台

Bw. Gao Weijie ni mtungaji muziki mashuhuri nchini ambaye alimaliza masomo katika chuo cha muziki cha Sichuan. Aliwahi kuwa mkurugenzi wa kitivo cha utungaji muziki cha chuo cha muziki cha Sichuan, mkurugenzi wa kitivo cha utungaji muziki cha chuo cha muziki cha taifa na mhariri wa jarida la “Muziki wa Umma”.

Mwaka 1983 Bw. Gao Weijie alianzisha kikundi cha kwanza cha muziki wa kisasa cha China kinachojulikana kwa “Jumuiya ya utafiti wa utungaji wa wanamuziki” na kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo. Hivi sasa Bw. Gao Weijie ni profesa wa chuo cha muziki cha taifa, msimamizi wa maalumu wa miradi ya utafiti wa idara ya utafiti wa taaluma ya muziki wa chuo cha muziki cha taifa, na kualikwa kuwa profesa wa chuo kikuu cha Yanbian na chuo kikuu kimoja nchini Marekani, na pia ni mhariri wa jarida la “Muziki wa China” na “Taaluma ya muziki wa China”.

Muziki aliotunga ulipinga nchini na katika nchi za nje na alipata tuzo nyingi. Muziki aliotunga ni pamoja na orchestra ya “mambo ya zamani kwenye mbuga”. Katika miaka ziaidi ya 40 Bw Gao Weijie alifundisha wanafunzi wengi ambao walipata tuzo nyingi katika mashindano ya utungaji muziki na baadhi yao wamekuwa watunga muziki mashuhuri. Bw. Gao Weijie alialikwa kutembelea New Zealand, Korea ya Kusini, Ufaransa, Uingereza, Marekani na nchi nyingine. Hivi sasa anapata kiinua mgongo maalumu kutoka kwa baraza la serikali.



  [Burudani za Muziki]Kutimiza Ndoto