Fu Lin
中国国际广播电台

Bw. Fu Lin alizaliwa tarehe 17 mwezi Januari mwaka 1946, mwaka 1968 alimaliza masomo katika kitivo cha muziki cha chuo cha sanaa cha jeshi la ukombozi la umma la China, alikuwa mchezaji wa ala za muziki, naibu kiongozi na mwongozaji wa sanaa wa kikundi cha nyimbo na ngoma cha jeshi la baharini la China, vile vile alikuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya jumuiya ya muziki ya China na kuwa naibu mwenyekiti wa jumuiya ya muziki wa kawaida ya China.

Katika miaka karibu 40 iliyopita alitunga nyimbo zaidi ya 1,000, lakini alisema kuwa hakuna wimbo aliotunga ambao unampendeza yeye mwenyewe. Alisema kuwa nyimbo wanazopenda watu ndio anazozipenda yeye.

Bw. Fu Lin alitunga muziki kwa ajili ya filamu zaidi ya 100 za sinema. Hivi sasa utungaji muziki ni moja ya kazi zake, na anatumia nafasi nyingi zaidi kufanya utafiti kuhusu nadharia ya muziki na kufundisha vijana wa muziki.

Katika mwaka 1986 na mwaka 1987 alifanya maonesho katika miji ya Haerbin na Xian, China ya nyimbo na muziki aliotunga yeye, ambayo ulioneshwa kwenye kituo cha televisheni cha CCTV mwaka 2001.  [Burudani za Muziki]Mbiu