Wang Luobin
中国国际广播电台

Bw. Wang Luobin (1913-1996) anasifiwa kama ni mwenezaji wa nyimbo za jadi za sehemu ya magharibi ya China na bingwa wa nyimbo za mtindo wa kisasa nchini China. Alizaliwa Beijing mwezi Januari mwaka 1913. Harakati za utamaduni mpya zilipojitokeza mwaka 1919 wakati alikuwa akisoma katika shule ya msingi, alianza kujifunza baadhi ya nyimbo za nchi za magharibi na Japan. Mwaka 1924 Bw. Wang Luobin alisoma katika sekondari ya wamisionari, alishiriki kwenye kikundi cha kwaya ambapo alifahamu sauti zinazolingana za nyimbo ( harmony ). Mwaka 1931 aliposoma katika chuo cha ualimu cha Beijing alijifunza uimbaji na kucheza piano kwa kumfuata mwalimu Bibi Horwath kutoka Urusi na kufundishwa muziki wa kijadi.

Mwaka 1937 Bw. Wang Luobin alishiriki kikundi cha sanaa kwenye medani ya sehemu ya kaskazini magharibi kilichoongozwa na mwandishi vitabu mashuhuri bibi Ding Lin. Mwaka 1938 alipata uhamisho kwenda sehemu ya Xinjiang ambapo alisikia nyimbo nyingi za kupendeza za huko, akaanza kukusanya nyimbo za makabila madogo madogo.

Baada ya hapo Bw. Wang Luobin kila mara akifika katika sehemu mpya anajitahidi kukusanya nyimbo za jadi, kutokana na juhudi zake Bw. Wang Luobin amekusanya na kurekebisha nyimbo nyingi za Xinjiang, ambazo zinapendwa na watu hadi hivi sasa.

Kutokana na msingi wa kukusanya nyimbo za jadi, Bw. Wang Luobin alirekebisha baadhi ya nyimbo ambazo zilienea katika mikoa ya Gansu na Qinghai, kisha zikaenea katika sehemu mbalimbali nchini na katika miaka makumi kadhaa iliyopita nyimbo hizo zinapendwa na wachina wengi.  [Burudani za Muziki]Muziki wa Vijana