Lei Zhenbang
中国国际广播电台

Bw. Lei Zhenbang (1916-1997) ni mtungaji muziki wa sinema, aliwahi kuwa mratibu wa jumuiya ya wanamuziki ya China na mratibu wa jumuiya ya wacheza sinema wa China na kuwa mjumbe wa baraza la 6 la mashauriano ya kisiasa ya China. Bw. Lei Zhenbang alizaliwa mwezi Mei mwaka 1916 katika ukoo mmoja tajiri wa kabila la waman, alipenda kusikiliza opera ya Kibeijing, tangu alipokuwa na umri wa miaka 7 aliweza kuimba baadhi ya sehemu za michezo ya opera ya Kibeijing na nyimbo.

Mwezi Januari mwaka 1939 Bw. Lei Zhenbang alikwenda kusomea elimu ya muziki katika darasa la maandalizi kabla ya kuwa mwanafunzi wa chuo hicho cha muziki nchini Japan, na aliruhusiwa na mkuu wa shule kuwa mwanafunzi rasmi wa chuo cha muziki katika muda usiotimia nusu mwaka.

Bw. Lei Zhenbang alirejea nchini mwaka 1943 na kuwa mwalimu wa muziki katika sekondari ya wasichana ya Beijing na sekondari ya Huizhong mjini Beijing. Baada ya ushindi wa vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan, alianzisha kikundi cha simphony cha baada ya masomo chenye watu zaidi ya 50.

Bw. Lei Zhenbang alirekebisha muziki wa kale wa China ujulikanao kwa “wimbo wa huzuni” kuwa muziki wa orchestra kwa ajili ya maonesho ya bendi hiyo.

Mwezi Juni mwaka 1949 Bw. Lei Zhenbang alipata uhamisho kwenda kufanya kazi ya kutunga muziki katika kiwanda cha filamu za sinema cha Changchun.

Katika muda wa miaka zaidi ya 30 baada ya hapo alitunga nyimbo zaidi ya 100 kwa ajili ya filamu za sinema zinazopendwa na watu wengi, na baadhi yao zilipata tuzo za muziki.

Katika mwaka 1960, mwaka 1964 na mwaka 1980 muziki nyingi alizotunga zilipata tuzo za tungo bora.

Katika miongo kadhaa iliyopita muziki aliotunga kwa ajili ya filamu za sinema ikiwemo “Dong Cunrui”. “Dada wa tatu wa ukoo wa Liu” na “mgeni kutoka mlima wa wenye theluji” inapendwa sana na watu.  [Burudani za Muziki]Mbona Maua ni Mekundu Namna Hii