Zhang Li
中国国际广播电台

Mtungaji wa maneno ya nyimbo Bw. Zhang Li alizaliwa katika mji wa Dalian tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 1932. Mwaka 1948 alisoma kitivo cha fasihi katika chuo cha sanaa cha Lu Xun cha sehemu ya kaskazini mashariki. Mwaka 1955 alifundisha katika kitivo cha fasihi cha chuo kikuu cha ualimu cha Beijing na alihamishwa katika ofisi ya utungaji ya bendi ya ala za muziki za jadi cha taifa na kuwa mtungaji wa michezo wa ngazi ya kwanza ya taifa.

Katika miaka zaidi ya 50 iliyopita alitunga nyimbo nyingi zinazopendeza watu zikiwemo “kivuli cha fencing ”, “maisha yenye furaha na uchungu” na “Upepo wa Asia” ambazo zinapendwa sana na watu.

Bw. Hang Li alipita kwenye njia yenye shida nyingi hadi kufikia kwenye mafanikio. Katika miaka ya 60 ya karne ya 20 nyimbo alizotunga hazikupendwa na baadhi ya wataalamu na wanamuziki, lakini hakufa moyo, bali alijitahidi zaidi kuliko zamani, hatimaye alifanikiwa.

Hivi sasa ingawa amekuwa na umri wa miaka zaidi ya 70, na afya zake si nzuri sana, lakini bado ana shughuli nyingi, anaendelea kufanya kazi za utungaji, kushiriki katika semina na shughuli za kufundisha utungaji wa maneno ya nyimbo.  [Burudani za Muziki]Mimi na Taifa langu