Tian Han
中国国际广播电台

Tian Han ni mmoja ya watu waliojijengea msingi wa harakati za michezo ya kuigiza nchini China, na ni mtangulizi wa mageuzi ya michezo ya opera. Si kama tu alitunga michezo ya kuigiza na opera, bali alitunga michezo ya sinema, mashairi na nyimbo za sinema.

Bw. Tian Han alizaliwa tarehe 12 mwezi Machi mwaka 1898 katika ukoo wa wakulima mkoani Hunan. Bw. Tian Han alishiriki harakati za utamaduni mpya za kupinga ubeberu na umwinyi toka “vuguvugu la tarehe 4 Mei”. Alijiunga na chama cha kikomunisti cha China mwaka 1932, na baada ya hapo aliingia katika kipindi cha pili cha utungaji. Bw. Tian Han alitunga maneno ya wimbo wa jeshi la kujitolea ambao uliwahamasisha wachina wengi kushiriki kwenye vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan na kulikomboa taifa, wimbo huo ulifanywa kuwa wimbo wa taifa baada ya kuasisiwa kwa China mpya.

Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, Bw. Tian Han alikuwa kiongozi kwenye kazi yake, lakini hakuacha kazi ya utungaji. Mchezo wa historia aliotunga ujulikanao kwa “Guan Hanqing” ulionesha heshima yake kwa mtu huyo wa kale ambaye alimlalamikia Dou Er ambaye aliadhibiwa kwa makosa na kutendewa isivyo vya haki, lakini yeye mwenyewe aliteswa hadi kufariki dunia na “genge la watu wanne”. Mwaka 1968 aliugua ugonjwa na kupotea kutokana na kuteswa siku hadi siku.

Bw. Tian Han alitunga michezo ya kuigiza zaidi ya 60, michezo ya opera zaidi ya 20, sinema zaidi ya 10, mashairi zaidi ya 900 pamoja na insha na nyimbo nyingi.  [Burudani za Muziki]Songa Mbele Watu Mliojitolea