Xu Peidong
中国国际广播电台

Xu Peidong (1954--- ) mtungaji muziki mashuhuri wa China.

Bw. Xu Peidong alizaliwa katika mji wa Dalian tarehe 1 mwezi Februali mwaka 1954. mwaka 1970 alifaulu mtihani wa kuingia katika kikundi cha nyimbo na ngoma cha eneo la jeshi la Fuzhou na kuwa mpiga fidla kubwa wa kwanza, mwelekezaji wa bendi na mtunga muziki. Mwaka 1985 alikuwa mtunga muziki wa ngazi ya kwanza na naibu mwenyekiti wa jumuiya ya muziki mwepesi ya China. Mwaka 1992 na mwaka 1996 aliteuliwa kuwa mmoja wa watungaji muziki wa China, na mwaka 1996 alipata “tuzo ya mafanikio ya utungaji muziki katika miaka 20” pamoja na “tuzo ya mafanikio ya utungaji wa nyimbo za mtindo wa kisasa za China”.

Alitunga muziki mwingi ikiwemo ya opera za “Hisia za jenerali”, “Maua ya mitende” na sinema ijulikanayo kwa “Vijana wa rock'n'roll” pamoja na muziki wa nyimbo nyingi zikiwa ni pamoja na “Mwezi wa tarehe 15 unapevuka zaidi tarehe 16”.



  [Burudani za Muziki]: Ardhi Kubwa ya Taifa