Qiao Yu
中国国际广播电台

Bw. Qiao Yu (1927---) mtungaji mashuhuri wa maneno ya nyimbo. Bw. Qiao Yu alizaliwa mwaka 1927 katika mji wa Jining mkoani Shandong ambaye anasifiwa kuwa ni bingwa wa utungaji wa maneno ya nyimbo nchini China. Mwaka 1946 alisoma katika chuo cha sanaa cha kaskazini mwa China. Aliwahi kuwa mtungaji wa opera tatu wa chuo hicho.

Baada ya China mpya kuasisiwa mwaka 1949, aliwahi kuwa mtungaji wa maneno ya nyimbo wa chuo cha michezo ya opera ya taifa, jumuiya ya watungaji wa michezo ya opera ya China na wa wizara ya utamaduni. Toka mwaka 1977 aliteuliwa kuwa naibu kiongozi na kiongozi wa kundi la michezo ya opera na ngoma la China, mratibu wa kituo cha kimataifa maingiliano ya utamaduni cha China. Alikuwa mjumbe wa baraza la 8 na mashauriano ya kisiasa la China.

Utungaji wa Bw. Qiao Yu unaendana na wakati, katika miaka ya 50 ya karne iliyopita alitunga michezo ya fasihi ya sinema ya “binti wa tatu wa ukoo wa Liu”, “Watoto Wekundu” maneno ya wimbo wa “Nchi Yangu”. Baada ya kuigia katika miaka ya 80, wakati ambapo China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi, Bw. Qiao Yu alitunga maneno ya nyimbo nyingi zikiwemo za “Waridi wa moyoni mwangu”, “Usiku wa leo usiosahaulika” pamoja na nyingi nyinginezo, ambazo zinapendwa na watu wengi.

Tungo nzuri zaidi za Bw. Qiao Yu ni pamoja na “Nchi Yangu”, “watu wanasifu mandhari nzuri ya Shanxi” na “waridi wa moyoni mwangu”.


  [Burudani za Muziki]Napenda Taifa Langu China