Nie Er
中国国际广播电台

Bw. Nie Er (1912---1935) mtunga mashuhuri wa muziki wa China.

Bw. Nie Er alizaliwa tarehe 14 mwezi Februali mwaka 1912 katika mji wa Kunming mkoani Yunnan, China. Mwaka 1918 alisoma katika shule ya msingi ya chuo cha ualimu cha Kunming. Alipata mafanikio mazuri katika masomo yake na alipenda sana muziki. Baada ya masomo alijifunza kupiga ala za muziki za jadi zikiwa ni filimbi, zeze la kichina na gambusi, hivyo anafahamu sana muziki ya jadi. Mwaka 1927 alifaulu mtihani na kusoma katika chuo cha kwanza cha ualimu mkoani Yunnan na kuanzisha “jumuiya ya muziki ya tisatisa” na kuanza kufanya maonesho chuoni na sehemu za nje, wakati ule alianza kujifunza fidla ya nchi za magharibi na piano.

Mwezi Novemba mwaka 1930 Bw. Nie Er alijiunga na “Umoja wa kupinga ubeberu”. Mwezi Machi mwaka 1931 alikuwa mpiga fidla katika kikundi cha opera cha Mingyue. Mwezi Aprili mwaka 1932 alifahamiana na mtungaji wa michezo ya opera na mshairi Bw. Tian Han, kutokana na kuathiriwa naye Bw. Nie Er alikwenda Beijing mwezi Agosti mwaka 1932 na kujiunga na umoja wa wanamuziki wa mrengo wa kushoto, na kujifunza kupiga fidla kutoka mwalimu wa kigeni Bw. Tonov. Alirejea mjini Shanghai mwezi Novemba.

Baada ya kurejea Shanghai Bw. Nie Er alifanya kazi katika kampuni ya filamu za sinema ya Lianhua na alijitahidi kushiriki katika harakati za muziki, opera na sinema za mrengo wa kushoto. Aidha alishiriki katika shughuli za muziki za “Jumuiya ya marafiki wa Urusi” na kuanzisha “Jumuiya ya utafiti wa muziki ya Xinxing”.

Mwaka 1933 Bw. Nie Er alitunga muziki mpya wa mtindo mpya kabisa ukiwemo ya “Wimbo wa uchimbaji madini” na “Wimbo wa uuzaji wa magazeti”. Mwaka 1934 alitengenezesha sahani za santuri za “Wimbo wa barabara kubwa”, “Watangulizi” na “Wimbo wa kuhitimu masomo”. Mwaka 1935 alitunga muziki wa nyimbo za “Muziki wa Meiniang”, “Wasichana wa vijijini” na “Wimbo wa kusonga mbele wa jeshi la kujitolea” ambao ulikuwa wimbo wa taifa baada ya kuasisiwa China mpya.

Tarehe 18 mwezi Aprili mwaka 1935 Bw. Nie Er aliwasili Tokyo, Japan ambapo alifanya uchunguzi kuhusu muziki, michezo ya opera na sinema, aliwafahamisha sekta ya fasihi na sanaa ya Japan kuhusu maendeleo mapya ya muziki nchini China, na alijifunza lugha na muziki wa Japan. Bw. Nie Er alifariki katika maji nchini Japan tarehe 17 mwezi Julai alipokuwa na umri wa miaka 23 tu.

Bw. Nie Er alikuwa na muda wa miaka kiasi cha miwili ya kutunga muziki, lakini alitunga muziki wa aina 20 hivi kwa ajili ya nyimbo za filamu 8 za sinema, michezo mitatu ya kuigiza na opera moja. Licha ya hayo alitunga muziki wa aina 41 ukiwa ni pamoja na nyimbo 15 na muziki wa aina nne wa ala za jadi.

 

  [Burudani za Muziki]Wimbo wa Taifa