Liu Tianhua
中国国际广播电台

Bw. Liu Tianhua (1895---1932) alikuwa mtungaji muziki mashuhuri, mwanamuziki na mwalimu wa ala za muziki za jadi. Bw. Liu Tianhua alizaliwa mwaka 1895 katika ukoo wa msomi wa wilaya ya Jiangyin, mkoani Jiangsu. Ndugu watatu wa ukoo huo wote ni hodari. Mwaka 1912 Bw. Liu Tianhua alishiriki kwenye bendi moja mjini Shanghai, na kujifunza nadharia ya muziki, piano, fidla na za aina nyingine. Alirejea kwao mwaka 1914 na kufundisha masomo ya muziki katika shule moja ya sekondari.

Mwaka 1915 Bw. Liu Tianhua alifiwa na baba yake, ambapo katika majonzi makubwa alitunga muziki “kupiga kite”, na kuanza kushika njia ya utungaji wa muziki.

Ili kujifunza muziki ya jadi ya China Bw. Liu Tianhua aliwatembelea wanamuziki wa jadi na kujifunza kutumia ala za muziki za kijadi. Alifanya mageuzi kuhusu upigaji wa zeze la kijadi na kufanya upigaji wa ala hiyo ya muziki kuoneshwa katika maonesho ya muziki na kufundishwa katika vyuo vya muziki.

Katika miaka 10 ya kutoka mwaka 1922 hadi 1932, Bw. Liu Tianhua alikuwa profesa wa ala za muziki za zeze ya kijadi, gambusi na fidla. Katika utungaji wa muziki alirithi ufundi wa utungaji wa muziki wa kijadi huku akijifunza mbinu ya utungaji wa muziki ya nchi za magharibi.

Toka alipokuwa na umri wa miaka 17 Bw. Liu Tianhua alianza kufundisha muziki katika shule za msingi na sekondari, na alikuwa na uzoefu mwingi wa kufundisha, na aliweka msingi wa mfumo wa elimu ya muziki wa kijadi.

Alipoanza kuwa na mafanikio makubwa Bw. Liu Tianhua alianza kuugua, mwezi Mei mwaka 1932. Wakati alipofariki alikuwa na umri wa miaka 38 tu.

Muziki safi aliotunga Bw. Liu Tianhua ni pamoja na “Kupiga kite”, “wimbo wa majonzi” na “Usiku mwema”.  [Burudani za Muziki]Usiku wenye Furaha