Yan Liangkun
中国国际广播电台

Mwongozaji wa bendi Bw. Yan Liangkun alikuwa naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wanamuziki ya China, mratibu mkuu wa jumuiya ya waongozaji wa kwaya na mwongozaji wa benki ya taifa. Alizaliwa katika mji wa Wuhan mwaka 1923. Mwaka 1942 alisoma katika kitivo cha nadharia cha chuo cha muziki wa taifa, mwalimu wake wa muziki alikuwa profesa Jiang Dingxian na alijifunza uelekezaji wa bendi kwa kumfuata Bw. Wu Bochao. Mwaka 1947 alihitimu masomo yake na kwenda kufanya utafiti wa nadharia katika chuo cha muziki cha China mjini Hong Kong na kufundisha uongozaji wa bendi katika chuo hicho.

Baada ya China mpya kuasisiwa mwaka 1949, Bw. Yan Liangkun alifundisha muziki katika chuo cha muziki cha taifa na kuwa mwelekezaji wa bendi ya kwaya wa kikundi cha waimbaji vijana cha chuo hicho, na alikuwa mwongozaji wa kikundi cha kwaya cha taifa mwaka 1952. alikwenda Urusi kuchukua mafunzo mwaka 1954, aliporejea nchini mwaka 1958 alikuwa mwelekezaji wa kikundi cha kwaya cha taifa.

Mwaka 1983 kamati ya Kodaly ya Hungary ilimtunukia shahada na medali ya kumbukumbu kutokana na mchango aliotoa katika kuwafahamisha watu muziki na mafunzo ya Kodaly. Alishiriki kwenye matamasha mengi ya muziki. Mwaka 1986 aliteuliwa kuwa mjumbe wa kudumu katika tamasha la pili la kwaya mjini Beijing na kuwa kiongozi wa tamasha hilo. Kikundi cha kwaya cha taifa alichoongoza kilipata nafasi ya kwanza ya tuzo ya ngazi ya kwanza katika “tamasha la kwaya la Beijing.”

Bw. Yan Liangkun aliongoza kikundi cha waimbaji kufanya maonesho na alialikwa kwenda kuongoza bendi Amerika ya kaskazini, Asia ya Kusini Mashariki, Taiwan na Hong Kong, na mara kwa mara alikwenda sehemu mbalimbali nchini kufundisha muziki.

 

  [Burudani za Muziki]Kwaya ya Kusifu Mto Manjaro