Piao Dongsheng
中国国际广播电台

Bw. Piao Dongsheng alizaliwa mwaka 1934 katika mji wa Shenyang mkoani Liaoning, tangu mwaka 1949 alifanya kazi za sanaa na alikwenda kusoma katika chuo cha fasihi na sanaa cha Lu Xun. Bw. Piao Dongsheng alikuwa mwelekezaji wa ngazi ya kwanza ya taifa wa kikundi cha nyimbo na ngoma cha taifa na kuwa kiongozi wa shirika la uchapishaji wa audio na video. Hivi sasa yeye ni kiongozi wa jumuiya ya muziki wa orchestral wa jadi ya taifa na mjumbe wa kamati ya uelekezaji wa wataalamu wa mtihani wa kiwango cha sanaa ya jamii ya wizara ya utamaduni.

Shughuli muhimu alizofanya Bw. Piao Dongsheng katika miaka zaidi ya miaka 50 iliyopita zilikuwa kuongoza bendi ya orchestral ya jadi. Aliwahi kuongoza bendi yenye wanamuziki elfu moja katika “maonesho makubwa ya China” ya tamasha ya kwanza ya sanaa ya China. Aliwahi kualikwa kufanya kazi za kuongoza bendi za ala za muziki za jadi ya Taibei, Gaoxiong, Hong Kong, Singapore, Chengdu na bendi ya ala za muziki za jadi ya kikundi cha nyimbo na ngoma cha taifa.

Licha ya kuelekeza bendi, vilevile alifanya kazi za kutunga muziki na utafiti wa nadharia ya muziki. Alitunga nyimbo karibu 100 ukiwemo “Muziki ya jadi ya Jiangsu”, “kusherehekea ushindi” na “kwenye mbuga”.

Mwaka 1993 aliteuliwa na wizara ya utamaduni ya China kuwa mtaalamu aliyetoa mchango mkubwa, na kupewa kiinua mgongo maalumu na serikali.


  [Burudani za Muziki]Heri na Baraka