Hu Bingxu
中国国际广播电台

Bw. Hu Bingxu ni mmoja wa waongozaji hodari wa bendi nchini China. Mwaka 1958 alishinda mtihani na kujifunza muziki wa orchestral katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1959 aliteuliwa kujifunza oboe katika darasa la wataalamu nchini Jamhuri ya Czech. Baada ya kumaliza masomo yake mwaka 1963 alikuwa mpiga oboe katika bendi ya symphony ya taifa.

Kwa nyakati mbalimbali Bw. Hu Bingxu alikuwa mwongozaji wa bendi na sanaa katika vikundi 7 vya ngazi ya taifa.

Aliwahi kushiriki maandalizi ya maonesho ya muziki wa symphony yakiwemo “Shajiabang” na “Mlima wa Cuckoo”.

Kutokana na mafanikio aliyopata Bw. Hu Bingxu katika shughuli za uongozaji wa bandi alipewa tuzo na wizara ya utamaduni. Mwaka 1995 Bw. Hu Bingxu alipata tuzo maalumu ya “sahani ya dhahabu ya santuri”.

Anaongoza bendi kwa ustadi na miondoko maridali, hususan yeye ni hodari sana kuhamasisha hisia za wanamuziki na maingiliano kati ya muziki na wasikilizaji. Sahani tatu zilizochapishwa mara ya kwanza na kampuni ya Philips katika China bara zilipigwa na bendi zilizoongozwa naye.

Bw. Hu Bingxu anazingatia kuendana na maonesho ya muziki na kuyapeleka katika mazingira mapya kabisa, na kuinua kiwango ustadi wa kuelekeza benki za ala za jadi katika kiwango cha ustadi wa uongozaji wa bendi wa kiwango cha juu duniani.

Mwaka 1999 aliongoza bendi ya ala za muziki za jadi ya taifa kufanya maonesho katika miji 18 ya Marekani na kufanya ushirikiano na mpiga fidla Ma Youyou ambaye ni mwanamuziki wa ngazi ya juu duniani, ambapo alipata mafanikio makubwa katika maonesho ya muziki uitwao “Ndoto ya Spring” yaliyofanywa katika ukumbi wa muziki wa Carnegie.


  [Burudani za Muziki]Dansi ya Panda