Chen Xiyang
中国国际广播电台

Bw. Chen Xiyang alijifunza utungaji wa muziki mwaka 1960 katika chuo cha muziki. Alihitimu masomo kwa mafanikio mazuri mwaka 1965 na kuwa mwongozaji wa bendi ya orchestral ya kikundi cha ballet cha Shanghai. Tokea miaka ya 70 alifanya maonesho katika nchi nyingi zikiwemo Korea ya Kaskazini, Japan, Canada na Ufaransa.

Mwaka 1981 Bw. Chen Xiyang alijifunza uongozaji wa bendi katika Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani, baada ya hapo alifanya ushirikiano na bendi za New York, Brooklyn na bendi ya Honolulu katika maonesho ya muziki.

Mwaka 1982 alialikwa kuongoza bendi katika tamasha la muziki ya Asbon, Marekani. Hapo baadaye alialikwa na kampuni ya sahani za santuri ya “Sauti ya Muziki” na kuongoza bendi ya symphony ya taifa ya Beijing kurekodi muziki ya mlango wa kwanza na wa nne wa Symphony ya Beethoven kwa ajili ya kutengenezesha sahani za santuri.

Toka mwaka 1985 Bw. Chen Xiyang alielekeza bendi ya kundi alilokuwa nalo au bendi za Urusi, Japan, Scotland, Italia, Uswisi, Hong Kong, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Macao, Marekani, Thailand, Singapore, Australia na Ujerumani kufanya maonesho ya muziki huko.

Mwaka 1897 alipata tuzo ya uongozaji bora wa bendi katika tamasha ya muziki ya “Spring ya Shanghai” na muziki wa “Liangzhu” alioongoza ulipata tuzo ya sahani za dhahabu mwaka 1989. Jina lake liliorodheshwa katika “Orodha ya majina ya watu mashuhuri duniani” lililochapishwa na kituo cha takwimu za kimataifa cha Cambridge cha Uingereza.



  [Burudani za Muziki]Mto wa Brahmaputra