Zheng Xiaoying
中国国际广播电台

Profesa Zheng Xiaoying ni mwongozaji muziki wa kwanza wa kike nchini China. Alikuwa mwongozaji wa kwanza wa kundi cha opera la taifa na mkurugenzi wa kitivo cha uongozaji wa muziki cha chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1981 alipata tuzo ya ngazi ya kwanza ya uongozaji muziki na idara moja ya wizara ya utamaduni.

Mwaka 1947 alishinda mtihani wa kuingia chuo cha utibabu cha consonancy cha Beijing na kusomea elimu ya viumbe na muziki katika chuo cha wanawake cha Jinling. Mwaka 1948 alikwenda katika sehemu iliyokombolewa na kufanya kazi katika kikundi cha nyimbo na ngoma, mwaka 1952 alipelekwa kusomea utungaji wa muziki katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1955 alijifunza uelekezaji wa bendi na mwaka 1960 alikwenda kusoma nchini Urusi. Mwaka 1962 alifanikiwa kuelekeza bendi kupiga muziki wa opera ya Italia ijulikanayo kwa “Tosca” huko Moscow.

Tokea mwaka 1978 aliongoza bendi kufanya maonesho ya muziki ya kitaifa, ambapo aliongoza bendi kupiga muziki mwingi ya nchini na nchi za nje ikiwa ni pamoja na “bibi harusi wa mia moja”, “The Fallen Woman” na “Carmen”. Aidha, alishirikiana na bendi nyingi za nchini zikiwemo bendi ya muziki ya taifa, bendi ya symphony ya Shanghai, bendi ya symphony ya utangazaji na kundi la opera la taifa, muziki mwingi uliopigwa na bendi alizoongoza ulitengenezwa kuwa sahani za santuri.

Bibi Zheng Xiaoying ni mmoja wa profesa mwenye uzoefu mkubwa nchini katika eneo la uongozaji bendi za muziki. Wanafunzi wake kadhaa katika miaka ya karibuni walipata nafasi za mbele katika mashindano ya uelekezaji wa bendi ya kimataifa yakiwemo yale yaliyofanyika katika nchi za Marekani, Ufaransa, Italia, Austria, Jamhuri ya Czech na Ureno. Anapenda kueneza ufahamu wa elimu ya muziki kwa umma, na alifanya shughuli hizi mara karibu elfu moja, ambazo wasikilizaji wake wa moja kwa moja walikuwa zaidi ya laki mbili. Toka mwaka 1980 alifanya maonesho ya muziki zaidi ya 60 katika nchi za Japan, Marekani, Italia, Fenland, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji na Thailand, ambayo yalipendwa na watu wengi na kusifiwa na vyombo vya habari.



  [Burudani za Muziki]Dansi ya Taiwan