Li Delun
中国国际广播电台

Bw. Li Delun ni mshauri wa bendi ya symphony ya China, naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wanamuziki ya China. Mwaka 1917 alizaliwa katika Beijing, alijifunza upigaji wa piano na fidla alipokuwa mtoto, na aliposoma katika chuo kikuu cha Furen aliwashirikisha walimu na wanafunzi kuanzisha bendi ya orchestra na kufanya maonesho. Mwaka 1940 alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha muziki cha taifa mjini Shanghai, akaanza kujifunza upigaji wa fidla kubwa kutoka kwa mwalimu Shevtzov na mwalimu R. duckson na kujifunza nadharia ya muziki kutoka kwa mwalimu W. Frankel.

Mwaka 1942 yeye na wenzake walianzisha “Bendi ya symphony ya vijana ya China”. Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo cha muziki mwaka 1943 alikwenda kufundisha na kufanya kazi ya uongozaji wa bendi katika Yanan. Na alikuwa mwongozaji wa bendi katika kikundi cha opera cha taifa mjini Beijing mwaka 1949.

Mbali na kufanya maonesho katika sehemu mbalimbali nchini Bw. Li Delun aliongoza bendi ya symphony ya taifa kufanya maonesho nchini Japan, Korea ya Kaskazini, Hong Kong na Macao, licha ya hayo aliongoza bendi ndogo kufanya maonesho katika miji zaidi ya 20 nchini Hispania. Aliwahi kualikwa kuongoza bendi zaidi ya 20 za nchi za nje zikiwemo za Leningrad, Moscow na za nchi za Finland, Czech na Cuba. Mwaka 1987 alielekeza bendi kubwa yenye wanamuziki 800 katika tamasha ya muziki ya “Spring ya symphony ” yaliyofanyika mjini Beijing.

Baada ya mwaka 1985, Bw. Li Delun alikwenda kufanya maonesho ya muziki katika nchi za Luxembourg, Hispania, Ujerumani, Ureno, Canada na Marekani. Alielekeza bendi kupiga muziki iliyotungwa na wanamuziki mashuhuri zikiwemo “Kwaya ya mto Manjano” na “Wimbo wa misitu milimani”. Aidha aliwahi kufanya maonesho kwa ushirikiano na wanamuziki mashuhuri wa duniani na nchini.

Mwaka 1985 Bw. Li delunhuko Paris aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya mashindano ya upigaji fidla ya kimataifa, mwaka 1986 aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya mashindano ya fidla kubwa ya kimataifa ya Tchaikovsky yaliyofanyika huko Moscow.

Katika miaka mingi iliyopita, Bw. Li Delun alishughulikia uenezaji na maendeleo ya muziki wa symphony , alianzisha bendi katika miji zaidi ya 20 nchini ikiwemo Beijing na Tianjin na kuziandalia mafunzo.

Mwaka 1980 Bw. Li Delun alipata tuzo ya uongozaji wa bendi ya wizara ya utamaduni. Mwaka 1986 alipata medali ya kumbukumbu ya Liszt kutoka wizara ya utamaduni ya Hungry. Alifariki dunia tarehe 19 mwezi Oktoba mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 84.

) 

  [Burudani za Muziki]Muziki wa Mwanzo: Sikukuu ya Spring