Peng Xiuwen
中国国际广播电台

Bw. Peng Xiuwen ni mwelekezaji wa bendi na mtungaji muziki (1931-1996) alizaliwa mkoani Wuhan, alikuwa mwanamuziki mkubwa wa ala za muziki za jadi na mwongozaji wa kwanza wa bendi ya ala za muziki ya utangazaji ya taifa.

Bw. Peng Xiuwen alijifunza upigaji wa zeze la jadi na gambusi. Alihitimu masomo katika shule maalumu ya biashara mwaka 1949 na alifanya kazi katika kituo cha Radio cha Chongqing mwaka 1950.

Mwaka 1952 Bw. Peng Xiuwen alihamishwa katika bendi ya ala za muziki ya jadi, katika mwaka uliofuata alikuwa mwongozaji wa bendi na mtunga muziki.

Mwaka 1957 katika tamasha ya 6 ya vijana ya kimataifa iliyofanyika mjini Moscow bendi aliyoongoza ilipata medali ya dhahabu.

Mwaka 1981 kutokana na mwaliko wa bendi ya ala za muziki za jadi ya Hong Kong Bw. Peng Xiuwen alikuwa mwongozaji wa bendi hiyo. Katika mwaka huo aliteuliwa kuwa kiongozi wa sanaa wa bendi ya ala za muziki ya idara ya utangazaji ya China. Mwaka 1983 Bw. Peng Xiuwen aliteuliwa kuwa kiongozi wa bendi ya ala za muziki za jadi ya utangazaji ya China.

“Kuunganisha hisia zake na muziki na kuonesha hisia kwa muziki” ni sifa yake katika uongozaji wa bendi. Kutokana na kuongozwa naye, bendi hiyo ilichukua nafasi ya kwanza katika upigaji wa muziki wa ala za jadi.

Bw. Peng Xiuwen alitoa mchango mkubwa katika shughuli za muziki wa jadi, idadi ya muziki aliourekebisha na kutunga ni kati ya 400 hadi 500 hivi ikiwemo “Kwenye maua na mbalamwezi kando ya mto majira ya Spring” na “Muziki wa ngoma ya kabila la wa-yao”. Licha ya hayo alijaribu kupiga muziki mashuhuri wa nchi za nje kwa ala za muziki za kichina ikiwa ni pamoja na “ngoma ya Horo” na “Ruins of Athens” ya Beethoven”.

Baada ya kuingia miaka ya 80 ya karne iliyopita, Bw. Peng Xiuwen alitunga muziki mwingi na maarufu wa ala za muziki za jadi. Bw. Peng Xiuwen alifariki kutokana na kuugua tarehe 28 mwezi Desemba mwaka 1996 mjini Beijing.



  [Burudani za Muziki]Sifa ya Milele