Tang Can
中国国际广播电台

Mwimbaji mashuhuri Bw. Tang Can alizaliwa katika mji wa Zhuzhou, mkoani Hunan, alishinda mtihani wa kuingia kikundi cha nyimbo na ngoma cha taifa na kuwa mwimbaji wa kikundi hicho. Katika mashindano ya 7 ya televisheni ya waimbaji vijana ya China alipata tuzo ya “mwimbaji hodari”, na alipata tuzo katika mashindano ya 5 ya muziki wa televisheni ya “Kombe la Konka”.

Majira ya mwaka 1998 mafuriko makubwa yalitokea katika baadhi ya sehemu nchini China, licha ya kushiriki kwenye maonesho ya kuchangisha fedha alijigharimia upigaji filamu ya muziki wa televisheni “Mashujaa” kwa kuonesha heshima yake kwa mashujaa waliopamnana na mafuriko.

Mbali na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kikundi alichokuwepo, pia anashiriki kwenye shughuli za kuchangisha fedha kusaidia sehemu maskini na kutoa msaada kwa watoto walioacha masomo kutokana na matatizo ya kiuchumi kwenye familia zao.

Katika tamasha la michezo ya sanaa ya siku kuu ya mwaka mpya lililoandaliwa na televisheni ya taifa, wimbo walioimba Bw. Tang Can na mwenzake bibi Huo Feng ujulikanao kwa “Hali motomoto ya Mwanzoni” ulipendwa sana na wasikilizaji na kutengenezwa kuwa video. Katika tamasha la kukaribisha milenia mpya lililofanyika mwaka 2000, waliimba tena wimbo huo na kupata pongezi kubwa.

Ili kuadhimiisha miaka 50 ya China mpya, wimbo alioimba Bw. Tang Can “Ninalitakia kila la heri taifa langu”, ambao ulitungwa na mwanamuziki Bw. Meng Qingyun, ulitengenezwa kuwa MTV, wimbo huo ulipendwa na watu wengi, wimbo huo uliimbwa pia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya China mpya zilizoandaliwa na vituo vya televisheni vikiwemo vya mikoa ya Hunan, Hubei, Zhejiang na mji ya Shanghai.

Wimbo wa “Ninalitakia kila la heri taifa langu” ulipata tuzo ya wimbo bora na kupata tuzo ya dhahabu ya muziki wa televisheni.

Mwaka 2000 Bw. Tang Can aliimba wimbo uliotungwa na mwanamuziki Fu Ke “Furaha Milele” katika kipindi cha “Wimbo wa Wiki” cha Televisheni ya taifa, ambao wimbo huo wa kienyeji uliimbwa kwa mtindo wa kisasa na kupendwa na watu wengi. Hapo baadaye Bw. Tang Can aliimba wimbo mwingine “Kwetu Maridadi”, ambapo umepongezwa sana na watu.

Mwaka 2001, Bw. Tang Can alipata tuzo ya dhahabu ya waimbaji wanaopendwa na wasikilizaji katika mashindano ya kwanza yaliyoandaliwa na idara kuu ya utangazaji ya China.



  [Burudani za Muziki]Tulitakie Taifa letu Ustawi na Neema