Yan Weiwen
中国国际广播电台

Bw. Yan Weiwen ni mwimbaji wa sauti ya juu ya kiume ya kikundi cha nyimbo na ngoma cha idara kuu ya siasa ya jeshi, mwanachama wa jumuiya ya waimbaji ya China, mwimbaji wa ngazi ya kwanza anayepata kiunua mgongo maalumu cha serikali.

Bw. Yan Weiwen alijifunza uimbaji kutoka kwa profesa Jin Tielin, tena anajifunza ubora wa waimbaji mbalimbali. Sauti yake ni nzito na kupendeza, sasa amekuwa mwimbaji hodari na kupendwa na watu

Bw. Yan Weiwen ametengeneza mkusanyiko wa nyimbo alizoimba na aliimba nyimbo kwa ajili ya makumi ya filamu zikiwemo za “Mfalme wa mwisho” na “Kikosi cha msalaba mwekundu”. Aliiwakilisha China kutembelea nchi na sehemu zaidi ya 20 zikiwemo Marekani, Japan, Canada, Ufaransa, Ujerumani na Italia, ambapo maonesho yake yalipendwa sana na watu wa huko.

Bw. Yan Weiwen alipata tuzo mara nyingi katika mashindano ya uimbaji ya taifa na ya jeshi, zikiwani pamoja na tuzo ya nafasi ya kwanza ya uimbaji wa jadi wa mashindano ya tatu ya waimbaji vijana ya China yaliyofanyika mwaka 1988, tuzo ya ngazi ya kwanza katika maonesho ya sanaa ya jeshi yaliyofanyika mwaka 1989.  [Burudani za Muziki]Mpopla Mdogo