Yang Hongji
中国国际广播电台

Bw. Yang Hongji ni mwimbaji mashuhuri wa China, mwanachama wa jumuiya ya wanamuziki ya China na mwanachama wa jumuiya ya wanamichezo ya opera ya China.

Bw. Yang Hongji alizaliwa katika mji wa Dalian mkoani Liaoning. Alipenda kuimba nyimbo tangu utotoni mwake, mwaka 1959 alijiunga na kikundi cha nyimbo na ngoma cha Dalian na alifaulu mtihani wa kujiunga na kikundi cha michezo ya opera cha idara kuu ya siasa ya jeshi mwaka 1962.

Bw. Yang Hongji alijifunza mwenyewe nadharia ya muziki anayopaswa kusoma mwanafunzi wa chuo cha muziki zikiwa ni pamoja na upigaji wa piano, elimu ya harmonic , mazoezi ya kuimba na kusikiliza pamoja na lugha ya Kitaliana. Vitu hivyo vimemsaida sana kupata mafanikio makubwa.

Mwaka 1979 mwongozaji mashuhuri wa bendi Bw. Seiji Ozawa wa Japan alifika China na kuonesha muziki wa Beethoven Symphony No. 9 kwa kushirikiana na bendi ya taifa ya China. Miongoni mwa makumi ya waimbaji nchini China, Bw. Yang Hongji aliteuliwa, uimbaji wake katika maonesho ulisifiwa na Bw. Seiji Ozawa. Mwaka 1984 kutokana na kupendekezwa na profesa Shen Xiang mwenye uraia wa Marekani alishirikiana na bendi ya Hong Kong na mwongozaji bendi Bw. Mo Yongxi aliimba nyimbo za zamani zinazojulikana kwa majira (seasons) kwa lugha ya Kingereza. Hususan ni kuwa katika mwaka 1998 alikuwa mhusika Qu Yuan katika mchezo wa opera aliotunga mwanamuziki Shi Guangnan unaojulikana kwa “Quyuan” na kupata mafanikio.

Bw.Yang Hongji alipata tuzo ya “Maua ya Plum” ya michezo ya opera ya taifa na tuzo kubwa “Wenhua” ya baraza la serikali. Na aliimba nyimbo za filamu za sinema makumi kadhaa zikiwemo “Hadithi ya Nchi Tatu” na “Kwa Heri Moscow”.

  

 [Burudani za Muziki]Mawimbi Makubwa ya Mto Changjiang yaelekea Mashariki