Lu Jihong
中国国际广播电台

Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo cha muziki cha Xian mwaka 1982, Bw. Lu Jihong alikuwa mwalimu wa muziki katika shule ya ualimu ya Lanzhou, alihamishwa katika kikundi cha nyimbo na ngoma cha Gansu mwaka 1985, na alijiunga na kikundi cha nyimbo na ngoma cha jeshi la baharini mwaka 1989.

Bw. Lu Jihong alipata nafasi ya kwanza mara tatu katika mashindano ya uimbaji ya mkoa wa Gansu, na alitapa nafasi ya pili katika mashindano ya uimbaji wa jadi ya waimbaji vijana ya China. Mwaka 1995 alipata tuzo ya dhahabu ya serikali katika mashidano ya nyimbo mpya ya utangazaji.

Katika miaka ya karibuni, licha ya kupata tuzo nyingi Bw. Lu Jihong aliimba nyimbo kwa ajili ya filamu zikiwemo “Majemedari wa Ukoo wa Yang” na “Kurejea Sichuan”. Uimbaji wake umejaa hisia na uhamasa unaonesha ilivyo mtindo wa uimbaji wa makabila mbalimbali. Alikuwa mhusika katika opera ya “Marijani nyekundu”, na kushiriki tamasha la uimbaji la Televisheni ya taifa na mikoa.

Mwaka 2001 katika mashindano ya muziki wa MTV ya Televisheni, “Wimbo wa China kusonga mbele” alioimba pamoja na wenzake wengine wawili kwa pamoja ulipata tuzo ya dhahabu.

Bw. Lu Jihong akiwakilisha China na jeshi alitembelea Ujerumani, Urusi, Philippines, Thailand na Marekani na kupendwa na watu wa huko.


  [Burudani za Muziki]Wananchi Waishi kwa Usalama na Utulivu