Liao Changyong
中国国际广播电台

Bw. Liao Changyong ni mmoja wa waimbaji wachache wanaofanya maonesho katika jukwaa la kimataifa. Yeye alijifunza uimbaji kutoka kwa mwalimu Zhou Xiaoyan na mwimbaji wa kiume wa sauti ya juu Bw. Luo Wei, mwaka 1995 alihitimu masomo yake na kupata shahada ya pili katika chuo cha muziki cha Shanghai.

Katika miaka ya karibuni Bw. Liao Changyong alipata tuzo nyingi kubwa za mashindano ya uimbaji duniani yakiwemo mashindano International Toulouse Singing, Placido Domingo Opera World na Queen Songja International Music.

Katika miaka ya karibuni Liao Changyong alialikwa Bw. Placido Domingo kushirikiana naye kufanya maonesho katika tamasha ya muziki ya mwaka mpya huko Tokyo. Muda si mrefu uliopita Bw. Liao Changyong aliimba upya opera ya Maria Stuarda kwenye ukumbi wa Carnegie, uimbaji wake ulipendwa na wasikilizaji wanaopenda kutoa ukosoaji kuhusu waimbaji.

Akiwa mwanafunzi anayependwa sana na mwalimu wake Bw. Domingo, alialikwa na mwalimu huyo kufanya maonesho katika sehemu nyingi duniani. Mwaka 2001 alifanya ushirikiano tena na Bw. Domingo kuimba opera ya Offenbach. Mwaka 2002 Bw. Domingo alimwalika tena kufanya maonesho katika sherehe ya kuadhimisha miaka 10 ya mashindano ya opera ya kimataifa ya Domingo.

Hivi sasa, Bw. Liao Changyong ni profesa wa chuo cha muziki cha Shanghai na kuwa mkurugenzi wa kitivo cha uimbaji.  [Burudani za Muziki]Waache Wenye Haraka Wapite (Kutoka Opera ya Kinyozi M-serbia)