Guo Lanying
中国国际广播电台

Bibi Guo Lanying ni mwimbaji maarufu sana nchini China. Alizaliwa mwezi Desemba mwaka 1930 katika ukoo wenye matatizo ya kiuchumi mkoani Shaxi. Alipokuwa na umri wa miaka 6 alikwenda kujifunza uimbaji wa opera ya Zhonglubangzi, na alianza kufanya maonesho alipokuwa na umri wa miaka 7. Opera za jadi alizoimba ni zaidi ya 100, na alianza kujulikana nchini.

Katika majira ya Autumn mwaka 1946 aliondoka katika kikundi cha Opera ya Zhangjiakou na kushiriki kwenye kikundi cha wasanii cha Lianda kilichoko sehemu ya kaskazini ya China na kuanza kuimba opera za kisasa.

Mwaka 1947 bibi Guo Lanying alikuwa akisoma katika idara ya opera ya chuo kikuu cha Lianda huku akishiriki kwenye maonesho. Mwezi Agosti mwaka 1948 alijiunga na kikundi cha kwanza cha sanaa cha chuo kikuu hicho, ambapo maonesho yake yalipendwa na watu. Mwezi Aprili mwaka 1949 alishiriki kwenye ujumbe wa vijana wa China na kufanya maonesho katika tamasha la 2 la kimataifa la amani na urafiki la wanafunzi vijana huko Hungary na kupata tuzo.

Mwaka 1949 baada ya kuasisiwa kwa China mpya, bibi Guo Lanying alikuwa mhusika katika vikundi vya michezo ya opera, na kuwa mjumbe wa shirikisho la nne la utamaduni la taifa, aliimba opera nyingi maarufu na kuwa mwimbaji aliyependwa na watu wengi. Bibi Guo Lanying alishiriki kwenye ujumbe wa China na kutembelea nchi kiasi cha 20 zikiwemo Urusi, Romania, Poland, iliyokuwa inaitwa Czechoslovakia, Yugoslavia, Italia na Japan.

Bibi Gu Lanying aliacha kuimba kwenye jukwaa la muziki mwaka 1982 na kuwa mwalimu wa chuo cha muziki cha China. Mwaka 1986 alianzisha shule ya sanaa ya Guo Lanying huko Guangdong na kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo. Mwaka 1989 alipata tuzo ya sahani ya dhahabu kwenye mashindano ya kwanza ya taifa.

Sauti ya Guo Lanying ni nyororo na pana. Alipokuwa msichana alipewa mafunzo makali ya opera, hivyo ana msingi madhubuti wa sanaa. Nyimbo zake zinazopendeza zaidi ni pamoja na “wimbo wa uhuru wa wanawake”, “Shangazi Wang anataka amani” na “Mito na milima” ya opera ya Liu Hulan.

  [Burudani za Muziki]Taifa Langu