Zhang Ye
中国国际广播电台

Bibi Zhang Ye alizaliwa mkoa wa Hunan, hivi sasa yeye ni mwimbaji hodari wa nyimbo za jadi za China. Alimaliza masomo yake mwaka 1991 katika chuo cha muziki cha China, mwaka 1995 alipata shahada ya pili, sasa yeye ni mwalimu kijana wa uimbaji katika chuo cha muziki cha China.

Mwaka 1988 Zhang Ye alichukua nafasi ya tatu katika mashindano ya taifa ya televisheni ya waimbaji vijana na alipata tuzo ya dhahabu ya mashindano ya waimbaji hodari ya taifa. Tokea mwaka 1980 hadi mwaka 1995 alipata tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na medali ya fedha katika mashindano ya 4 ya taifa ya muziki wa MTV ya China na tuzo ya medali ya dhahabu ya mashindano ya muziki wa MTV ya kombe la Konka.

Katika masomo na maonesho yake Zhang Ye alikuwa mhusika mkuu katika opera nyingi, vilevile aliimba nyimbo nyingi kwa ajili ya filamu za sinema. Aidha, alifanya maonesho katika Uingereza, Ufaransa, Uswisi, Ujerumani, Sweden, Ubelgiji, Luxembourg, Japan na nchi za Asia ya kusini mashariki.

Bibi Zhang Ye anafaa kuimba nyimbo za jadi za mitindo mbalimbali, sauti yake ni nyororo, tulivu na wazi. Kuna waelezaji wa muziki ambao walisema kuwa sauti ya nyimbo ya bibi Zhang Ye ni kama maji ya theluji ya mlimani, safi na tamu.  [Burudani za Muziki]Kuingia Kwenye Enzi Mpya