Wu Bixia
中国国际广播电台

Bibi Wu Bixia ni mwimbaji mwenye sauti ya juu ya mtindo wa nchi za magharibi. Alizaliwa mkoani Hunan na alipokuwa na umri wa miaka 12 alianza kufanya maonesho ya uimbaji. Kutokana na kipaji chake na kufanya mazoezi kwa bidii anaweza kuimba nyimbo za jadi za China pamoja na nyimbo za nchi za magharibi.

Bibi Wu Bixia alipata tuzo nyingi zikiwa ni pamoja na tuzo ya fedha katika mashindano ya uimbaji yaliyoandaliwa na jumuiya ya wanamuziki ya China na wizara ya utamaduni ya China kwa pamoja mwaka 1993, tuzo ya nafasi ya kwanza ya uimbaji wa jadi katika mashindano ya uimbaji ya taifa mwaka 1996, tuzo ya nafasi ya kwanza katika mashindano ya uimbaji ya kimataifa yaliyofanyika nchini China. Tuzo ya nafasi ya kwanza ya mashindano ya uimbaji ya kimataifa yaliyofanyika huko Bicbao nchini Hispania na tuzo ya nafasi ya pili katika mashindano ya uimbaji ya kimataifa ya Tchaikovsky, ambayo yanachukuliwa kuwa ni mashindano ya “Olimpiki” ya waimbaji duniani.

Toka mwaka 2000 bibi Wu Bixia alifanya maonesho yake ya uimbaji katika Beijing, Hunan, na Singapore, licha ya hayo alifanya ushirikiano na bendi za nchini na duniani katika maonesho ya muziki. Mwezi Desemba mwaka 2001 kutokana na mwaliko wa kamati ya maandalizi ya uimbaji wa kimataifa na jumba la opera ya Arriaga la Hispania alikuwa mhusika mkuu wa kike katika opera ya Rigoletto.

Mafanikio ya uimbaji ya bibi Wu Bixia yamefuatiliwa na vyombo vya habari vya China na duniani, CCTV ilitengenezesha video ya uimbaji wake, magazeti ya Hispania yalimsifu kuwa na “Sauti iliyotoka mbinguni”, vyombo vya habari vya Russia vilimsifu kuwa ni “malaika mwimbaji aliyetoka mashariki”.


  [Burudani za Muziki]Chiriku