Cheng Zhi
中国国际广播电台

Bw. Cheng Zhi ni mwimbaji wa sauti ya juu, yeye ni mwanachama wa jumuiya ya wanamuziki ya China na mwimbaji wa ngazi ya kwanza wa kikundi cha nyimbo na ngoma cha idara ya kuu ya siasa ya jeshi. Alizaliwa mwaka 1946, aliingia katika kikundi hicho cha nyimbo na ngoma mwaka 1965, alihitimu masomo yake katika chuo cha muziki cha taifa.

Maneno katika nyimbo alizoimba yanasikika vizuri, sauti yake ni madhubuti na wazi. Anafahamu sana uimbaji wa jadi wa Italia, vilevile anaweza kuimba vizuri nyimbo za jadi za China. Alikuwa mhusika mkuu katika opera ya “Shangshi” iliyotungwa na mtunzi hayati Shi Guangnan na alisifiwa na wataalamu wa nchini na wa nchi za nje.

Mmoja wa waimbaji mashuhuri wa kike duniani ambaye ni kiongozi wa kundi la opera ya New York, Marekani bibi Bevery Bechi alimsifu kuwa ni “mmoja wa waimbaji wachache sana wa sauti ya juu na ni mwimbaji wa mtindo wa kweli wa Italia”.

Katika miaka ya karibuni Bw. Cheng Zhi alifanya maonesho mara nyingi katika sehemu mbalimbali duniani akiwa msanii wa China, vilevile alifanya maonesho ya uimbaji katika miji mingi ambayo ni pamoja na Beijing, Shanghai, Guangzhou, Shenzhen na Hong Kong.

  [Burudani za Muziki]Ah, Jua Langu