Song Zuying
中国国际广播电台

Bibi Song Zuying (1966--- ) ni mmoja wa waimbaji vijana hodari nchini China. Alizaliwa tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1966 katika kijiji cha wa kabila la wamiao chenye koo tatu mkoani Hunan. Mwezi Julai mwaka 1981 bibi Song Zhuying alimaliza masomo yake katika shule ya sekondari na kuchaguliwa na kikundi cha michezo ya opera cha wilaya. Baada ya muda usiotimia mwaka mmoja alishinda mtihani wa kuingia katika kitivo cha nyimbo na ngoma cha chuo cha makabila madogo cha taifa ambapo alimaliza masomo yake mwaka 1987. Mwezi Oktoba mwaka 1988 katika mashindano ya taifa ya “kombe la Jinlong” bibi Song Zuying alipata tuzo ya dhahabu kwa wimbo alioimba wa “kaka usiondoke”. Mwaka 1991 alihamishwa katika kikundi cha nyimbo na ngoma cha jeshi la baharini, sasa yeye ni mwimbaji wa ngazi ya kwanza wa taifa na kupewa kiinua mgongo cha serikali.

Sauti ya bibi Song Zuying ni nyororo, tamu na pana. Mizizi yake ya sanaa inaota katika udongo wa uimbaji wa nyimbo za jadi ya China na kuchanganya mtindo wa uimbaji wa nchi za magharibi ambavyo vimekuwa umaalumu wake. Nyimbo za kichina alizoimba ambazo ni pamoja na “Kikapu cha Mwanzi”, “Dada shupavu” na “Maisha Mazuri” zinapendwa na wachina nchini na nchi za nje.

Mwaka 2000 alipata “Tuzo Kubwa ya Nyimbo za Jadi za Wachina” mwaka 2002 alifanya maonesho ya muziki huko Sydney Opera House, na mwaka 2003 alifanya maonesho ya uimbaji wa solo kwenye Golden Concert Hall.  [Burudani za Muziki]: Maisha Mazuri