Jiang Dawei
中国国际广播电台

Jiang Dawei (1947---): Mwimbaji mashuhuri nchini China.

Bw. Jiang Dawei alizaliwa mwaka 1947 katika mji wa Tianjin. Tokea utotoni mwake alipenda muziki na uchoraji. Mwaka 1970 alijiunga na kikundi cha wasanii cha polisi wa misitu. Mwaka 1975 alikuwa mwimbaji wa solo katika kikundi cha nyimbo na ngoma za jadi cha taifa, hapo baadaye alikuwa kiongozi wa kikundi hicho na kiongozi wa bendi ya muziki mwepesi ya China.

Katika miaka mingi iliyopita aliimba nyimbo zaidi ya 1,000 na aliimba nyimbo kwa ajili ya filamu zaidi ya 100 ambazo ni pamoja na “Mahali Panapochanua Maua ya Mipichi” na “Maua ya Peony”. Bw. Jiang Dawei amewahi kufanya maonesho katika Marekani, Canada, Japan, Ujerumani, Singapore na Thailand.

Nyimbo alizoimba na kupendwa na watu wengi ni pamoja na “Mahali Panapochanua Maua ya Mipichi”, “Wimbo wa Peony” na “Nauliza Njia Iko Wapi”.  [Burudani za Muziki]Sehemu yanapochanua Maua ya Peoni