Zhou Xiaoyan
中国国际广播电台

Zhou Xiaoyan (1918---) : Mwimbaji wa sauti ya juu ya mtindo wa jadi wa nchi za magharibi, mwalimu wa uimbaji na profesa wa chuo cha muziki cha Shanghai. Bibi Zhou Xiaoyan alizaliwa Mwaka 1918 katika ukoo wa wanaviwanda na wafanya-biashara mjini Wuhan. Baba wa Zhou Xiaoyan alikuwa mwanakiwanda aliyependa sana muziki, kutokana na athari ya baba yake, Zhou Xiaoyan alianza kupenda muziki tokea utotoni mwake.

Mwezi Septemba mwaka 1935 Zhou Xiaoyan alishinda mtihani na kuandikishwa na shule ya muziki ya Guoli mjini Shanghai. Mwaka 1937 ilipolipuka vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan, Bibi Zhou Xiaoyan aliacha masomo na kurejea kwao.

Mwishoni mwa mwaka 1938 bibi Zhou Xiaoyan alifika Paris na kujifunza uimbaji katika chuo cha muziki cha Urusi cha Paris. Mwezi Oktoba mwaka 1945 bibi Zhou Xiaoyan alifanya maonesho ya uimbaji kwenye jumba la opera ya taifa mjini Paris ambayo yaliwashangaza wasikilizaji wa Ufaransa. Hapo baadaye alialikwa kwenda Czech kushiriki tamasha la muziki lililojulikana kwa jina la “Spring ya prague”, ambapo alisifiwa kuwa ni “chiriku wa China”.

Mwezi Oktoba mwaka 1947 bibi Zhou Xiaoyan alirejea nchini China, wakati ule China ilikuwa chini ya utawala wa serikali ya chama cha Guomindang ambapo watu wa China waliishi maisha yenye shida kubwa. Mwaka 1949 China mpya iliasisiwa, bibi Zhou Xiaoyan aliajiriwa kuwa mwalimu wa uimbaji wa chuo cha muziki cha Shanghai.

Miaka kumi ya mapinduzi ya utamaduni ni kipindi chenye giza nene kabisa katika maisha ya bibi Zhou Xiaoyan, lakini upendo wake kwa muziki ulimfanya awe shupavu, mwimbaji maarufu wa sauti ya juu anayesifiwa kuwa mwimbaji wa kiwango cha kimataifa Bw. Wei Song ni mwanafunzi aliyefundishwa naye wakati ule.

Baada ya kumalizika kwa mapinduzi ya utamaduni, bibi Zhou Xiaoyan alianza tena kufundisha. Mwaka 1984 wanafunzi wake wanne walipata tuzo tatu za dhahabu na tuzo moja ya fedha katika mashindano ya uimbaji ya kimataifa yaliyofanyika huko Vienna. Mafanikio yao yaliwashangaza wanamuziki wa kimataifa.

Ili kustawisha uimbaji wa opera nchini China na kuimarisha maingiliano na ushirikiano wa utamaduni wa muziki wa kimataifa, mwezi May mwaka 1988 bibi Zhou Xiaoyan alianzisha kituo cha opera cha Zhou Xiaoyan katika chuo cha muziki cha Shanghai.

Katika miaka zaidi ya 50 iliyopita, waimbaji walioandaliwa na bibi Zhou Xiaoyan waliipatia China heshima kubwa. Baadhi ya wanafunzi wake wamekuwa waimbaji wa makundi ya Metropolitan Opera na San Francisco Opera nchini Marekani.



  [Burudani za Muziki]Utenzi wa Ukuta Mkuu