Hu Songhua
中国国际广播电台

Hu Songhua (1930---): Mwimbaji mashuhuri wa China

Mwaka 1930 Bw. Hu Songhua alizaliwa katika ukoo wa watu wa kabila la waman. Alijulikana alipokuwa kijana kutokana na nyimbo alizoimba za “Senjidema” na “wimbo wa mavuno makubwa”. Alianza kuwa mwimbaji wa kikundi cha nyimbo na ngoma za jadi cha taifa mwaka 1952.

Toka zamani sana Bw. Hu Songhua alivutiwa sana na nyimbo za makabila madogo madogo. Mwaka 1952 mchezo mkubwa wa ngoma “mashariki ni kwekundu” ulihitaji wimbo mmoja wa kabila la wamongolia, Bw. Hu Songhua alikabidhiwa jukumu hilo kutokana na kuwa anafahamu sana maisha ya watu wa kabila hilo. Hadi leo wasikilizaji bado hawawezi kusahau wimbo alioimba unaojulikana kwa “wimbo wa sifa”.

Bw. Hu Songhua aliwahi kuwa mhusika mkuu Asihaer katika opera ya “Aiguli” na mhusika mkuu wa kiume Ahe katika filamu ya muziki “Asima”. Aidha, aliimba nyimbo kwa ajili ya filamu za sinema karibu 30.

Mwaka 1992 Bw. Hu Songhua alishirikisha watu kupiga filamu 12 za nyimbo. Yeye mwenyewe alikuwa mwongozaji, msimamizi na mwimbaji mkuu, filamu hizo zinazoonesha sanaa za jadi za makabila madogo madogo zilipendwa na watu wengi.

Katika miaka mingi iliyopita, Bw. Hu Songhua alikwenda kukusanya nyimbo za jadi katika makabila zaidi ya 40, na amejulikana kutokana na uimbaji wake wenye hisia wazi na sauti nzuri.



  [Burudani za Muziki]Tunapenda Taifa Letu