Wang Ciheng
中国国际广播电台
Bw. Wang Ciheng ni mpigaji mashuhuri wa filimbi nchini China. Hivi sasa yeye ni mwanachama wa jumuiya ya wanamuziki ya China, jumuiya ya muziki wa orchestra ya China na mpiga ala za muziki wa bendi ya ala za muziki za jadi ya taifa.

Bw. Wang Ciheng alizaliwa mwaka 1959 katika mji wa Hangzhou mkoani Zejiang. Mwaka 1980 alijifunza upigaji wa filimbi katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1984 alihitimu masomo katika chuo cha muziki cha taifa akawa mpiga filimbi katika bendi ya ala za muziki ya taifa. Alifundishwa na walimu mashuhuri wa sehemu za kaskazini na kusini, hivyo ustadi wake wa upigaji filimbi ni kuunganisha umaalumu wa sehemu hizo mbili.

Muziki wa filimbi aliopiga unapendeza watu sana kutokana na sauti ya wazi, ya juu na yenye uchangamfu. Alipiga filimbi katika maonesho mengi makubwa ya muziki na alisifiwa na wanamuziki mashuhuri.

Uhodari wake katika upigaji filimbi ulimfanya apate tuzo mara nyingi katika mashindano ya muziki ya nchini na nchi za nje. Mwaka 1982 alipata tuzo ya ngazi ya tatu ya chuo cha muziki cha taifa, mwaka 1987 alipata tuzo ya ngazi ya kwanza katika mashindano ya kwanza ya muziki wa Guangdong ya taifa.

Mwaka 1990 Bw. Wang Ciheng alifanya maonesho ya upigaji filimbi kwenye ukumbi wa muziki wa Beijing na alisifiwa na wanamuziki wakubwa nchini China. Bw. Wang Ciheng aliiwakilisha China mara nyingi kutembelea Austria, Ufaransa, Ujerumani na Marekani, ambapo maonesho yake yaliwavutia watu wengi.

Bw. Wang Ciheng anatilia maanani sana kujifunza elimu ya utamaduni, hana ubaguzi juu ya vikundi vya sanaa vyenye mitindo mbalimbali, kitu anachofikiri ni namna ya kuimarisha umaalumu wa upigaji filimbi.  [Burudani za Muziki]Nguo Maridadi