Sheng Zhongguo
中国国际广播电台 

“Mwanamuziki mkubwa”, “Mpigaji wa fidla anayevutia zaidi” na “Menuhin wa China”, hizo ni sifa anazopewa Sheng Zhongguo na wanamuziki wakubwa duniani. Bw. Sheng Zhongguo ni mpigaji fidla (violin) wa ngazi ya taifa katika bendi ya symphony ya China na pia ni mmoja wa wapigaji fidla wa kwanza walioipatia heshima China duniani.

Bw. Sheng Zhongguo alizaliwa katika ukoo wa wanamuziki, wazazi wake ni wanamuziki, ambao watoto wao 10 kati ya watoto 11 ni wanamuziki, na watoto wao 9 ni wapiga fidla. Sheng Zhongguo ni mtoto wao wa kwanza, alizaliwa mwaka 1941.

Sheng Zhongguo alijifunza kupiga fidla kutoka kwa baba yake alipokuwa na umri wa miaka mitano, na alifanya maonesho ya kupiga fidla miaka miwili baada ya hapo. Alipokuwa na umri wa miaka 9 katika siku yake ya kuzaliwa Radio ya Wuhan ilirekodi muziki aliopiga Sheng Zhongguo na kutangazwa katika vipindi vyake, alisifiwa sana na wasikilizaji. Mwaka 1954 alisoma katika sekondari inayoendeshwa na chuo cha muziki cha taifa, katika maonesho ya muziki ya kuadhimisha miaka 200 tangu azaliwe Mozart Sheng Zhongguo alipiga fidla katika bendi iliyoongozwa na Li Delun.

Mwaka 1960, Bw. Sheng Zhongguo aliteuliwa kwenda kusoma kwenye shule ya muziki ya Tchaikovsky Conservatory mjini Moscow, ambapo alishiriki kwenye mashindano ya fidla ya kimataifa ya Tchaikovsky ya ngazi ya Olimpiki ya muziki duniani, alipata tuzo ya heshima, na kuwa mmoja wa wapiga fidla kwanza wa China waliopata tuzo katika mashindano ya kimataifa.

Mwaka 1964 Bw. Sheng Zhongguo alirejea nchini akawa mwanamuziki mashuhuri katika majukwaa ya muziki nchini na katika nchi za nje. Baada ya mwaka 1976 kila mwaka alifanya maonesho zaidi ya 100 katika sehemu mbalimbali duniani na kuwa mwanamuziki anayependwa sana na watu.

Toka miaka ya 80, Bw. Sheng Zhongguo alifanya maonesho mengi katika nchi mbalimbali duniani. Mwaka 1980 alifanya maonesho 12 ya muziki katika miji 6 nchini Australia, ambayo yalikuwa mnara katika historia ya maingiliano ya utamaduni kati ya China na Australia.

Toka mwaka 1987 Sheng Zhonguo kila mwaka alikwenda kufanya maonesho nchini Japan, alitoa sehemu fulani ya pato lake katika mfuko wa fedha za tiba za kusaidia wanafunzi wa nchi mbalimbali waliosoma nchini Japan, na serikali ya Japan ilimtunukia sifa ya “Balozi wa Utamaduni”. Kutokana na mchango aliotoa katika maingiliano ya utamaduni kati ya China na Japan, mwaka 1999 alipata tuzo iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya serikali ya Japan.

Sheng Zhongguo alisaini mikataba mingi ya maonesho na nchi za nje, shughuli za maonesho yake zimetoa mchango mkubwa kwa maingiliano ya utamaduni ya dunia. Mbali na hayo, alikwenda mara kwa mara kutoa mihadhara katika vyuo mbalimbali nchini ili kuhimiza maendeleo ya shughuli za muziki nchini.

Hivi sasa yeye ni mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la taifa, mjumbe wa kamati kuu ya umoja wa demokrasia, mratibu wa jumuiya ya wanamuziki ya China.



  [Burudani za Muziki]Wimbo wa Wanaoranda randa