Tang Junqiao
中国国际广播电台

Bibi. Tang Junqiao ni mpigaji filimbi kijana nchini China, hivi sasa yeye ni mpigaji filimbi wa kwanza wa bendi ya ala za muziki za jadi ya Shanghai. Tang Junqiao alijifunza kupiga filimbi kutoka kwa baba yake alipokuwa mtoto ambapo alipata mara kadhaa tuzo ya kwanza katika mashindano ya muziki ya vijana na watoto. Alipokuwa na umri wa miaka 16 alifanya maonesho ya upigaji filimbi wa solo. Hapo baadaye alijiunga na chuo cha muziki cha Shanghai. Mwaka 1966 bibi Tang Junqiao aliingia katika bendi ya ala za muziki wa jadi ya Shanghai na kuwa mpigaji filimbi wa kwanza wa bendi hiyo.

Bibi Tang Junqiao mwenye ustadi mkubwa wa kupiga filimbi, anashiriki mara kwa mara maonesho makubwa ya muziki na michezo ya sanaa ya televisheni yakiwemo “Maonesho ya muziki ya uchangishaji fedha ya milenia ya Hong Kong”, “Maonesho ya muziki ya mwaka mpya mwaka 2000 ya Shanghai” na “Maonesho ya muziki ya Spring mwaka 2001, Shanghai”.

Bibi Tang Junqiao amefuatiliwa na wanamuziki wa kimataifa, alialikwa kupiga filimbi kwa kushirikiana na Bw. Ma Youyou ambaye ni mpigaji maarufu wa fidla kubwa duniani katika kituo cha sanaa cha Babiken, na alisifiwa na watu wengi.

Katika sikukuu ya Spring ya China mwaka 2001 bibi Tang Junqiao alifuata bendi ya ala za muziki za jadi ya Shanghai kufanya maonesho ya muziki katika Golden Voncert Hall. Mwezi Julai mwaka huo alifanya maonesho ya upigaji filimbi huko Macao kutokana na mwaliko.

Alialikwa mara kwa mara kushiriki kwenye maonesho ya matamasha mengi maarufu yakiwa ni pamoja na tamasha la sanaa ya kimataifa la Osaka nchini Japan, tamasha la muziki la Ufaransa, tamasha la muziki la “Moto Kwenye Maji” mjini London, Tamasha ya muziki ya kimataifa mjini Beijing.

Bibi Tang Junqiao alifanya ushirikano mara kwa mara na bendi nyingi mashuhuri zikiwa ni pamoja na bendi ya symphony ya London na bendi ya symphony ya Ufaransa. Mbali na hayo aliwahi kutembela nchi za Marekani, Ujerumani, Japan, Uingereza Austria, Ubelgiji, Ufaransa na Italia.