Xue Wei
中国国际广播电台

Mpiga fidla mashuhuri ambaye alizaliwa mwaka 1963. Alipata mafunzo mazuri na kujenga msingi madhubuti. Mwaka 1981 alipata tuzo katika mashindano ya upigaji fidla ya China, mwaka 1982 alipata tuzo kwenye mashindano ya Carl Flesch International Violin.

Mwaka 1983 Bw. Xue Wei alifaulu mtihani wa kujiunga na chuo cha muziki cha taifa, na miaka miwili baadaye alikwenda kusoma nchini Uingereza. Mwaka 1986 alipata tuzo ya dhahabu ya fidla katika mashindano ya upigaji fidla ya Tchaikovsky mjini Moscow, katika mwaka huohuo alipata tuzo ya mwaka katika mashindano ya upigaji fidla ya vijana nchini Uingereza.

Baada ya kupata tuzo Bw. Xue Wei alisifiwa na pande nyingi. Jarida maarufu nchini Uingereza linalojulikana kwa jina la“Santuri” lilimsifu kuwa na “mmoja wa wapiga fidla hodari sana duniani”. Baada ya hapo alifanya maonesho mara kwa mara nchini Uingereza kwa kushirikiana na bendi nyingi kubwa za huko.

Toka mwaka 1989 Bw. Xue Wei aliajiriwa kuwa profesa katika chuo cha muziki cha kifalme cha Uingereza.



  [Burudani za Muziki]Hora Staccato