Zhao Songting
中国国际广播电台

Zhao Songting alizaliwa mwaka 1924 katika Dongyang, mkoa wa Zejiang, alipenda muziki tangu alipokuwa mtoto, na alianza kujifunza kupiga filimbi alipokuwa na umri wa miaka 9, muda si mrefu alifahamu kupiga ala za muziki za jadi za zeze la kichina, gambusi, zeze lenye nyuzi tatu na Suona. Baadaye alisoma katika chuo cha ualimu na alikuwa mwalimu wa muziki katika shule ya sekondari na chuo cha ualimu. Alipokuwa na umri wa miaka 22 baba yake alimtaka aache muziki na kusoma sheria katika chuo cha sheria cha Shanghai.

Mwaka 1949 Bw. Zhao Songting aliacha masomo ya sheria na alifaulu mtihani wa kujiunga na kikundi cha michezo ya sanaa, ambapo alifahamu upigaji wa ala kadhaa za muziki za nchi za magharibi. Mwaka 1956 aliandikishwa na kikundi cha nyimbo na ngoma za jadi cha mkoa wa Zejiang na alipata mafanikio katika maonesho ya kwanza ya wiki ya muziki ya taifa. Mwaka 1964 alipiga nyimbo mbili alizotunga yeye mwenyewe zinazojulikana kwa jina la ”Mandhari ya Mto Wu” na “Kuchuma Majani ya chai” ambayo ilisifiwa sana na wataalamu.

Hapo baadaye Bw. Zhao alianza kufanya utafiti wa kuhusu filimbi, kwa kusaidiwa na kaka yake ambaye ni mtaalamu wa fizikia alifanya majaribio kwa miaka mingi katika maabara, na hatimaye alitoa data za njia ya kisayansi ya utengenezaji wa filimbi.

Bw. Zhao Songting alipata mafanikio katika ufundishaji, na wanafunzi wake wengi wamekuwa watu mashuhuri nchini na katika nchi za nje. Mbali na hayo alifanikiwa katika utafiti wa aina mbili yaani filimbi inayopindika, hivyo urefu wa filimbi umeongezeka lakini upigaji wake bado ni rahisi; pili ni filimbi moja inatumika kama filimbi mbili.

Filimbi ya kichina ni maridadi na yenye sauti nzuri. Bw. Zhao Songting ameunganisha uzoefu wa upigaji filimbi wa sehemu za kusini na kaskazini na kufanya sauti yake kuvutia zaidi. Mbali na hayo ametumia maarifa ya kuvuta hewa ya kupiga ala ya suona katika upigaji wa filimbi.

Bw. Zhao Songting ana maoni ya kutumia ustadi wa muziki kutumikia kueleza maudhui ya muziki, ana wazo la kutumia uzoefu wa sehemu mbalimbali ili mradi vinaongeza uzuri wa muziki.

Ingawa Bw. Zhao alijifunza kupiga filimbi kutoka kwa wapigaji filimbi wala hakufundishwa katika chuo cha muziki, lakini ana elimu nyingi za fasihi ya sayansi, hivyo anaweza kufundisha vizuri, masomo ya darasani yametungwa kwa utaratibu mzuri, kwa hiyo wanafunzi wake wengi wamekuwa mabingwa wakubwa.

Ili kuendeleza muziki wa jadi, Bw. Zhao alikuwa anachapa kazi kwelikweli bila kujali uchovu. Bw. Zhao Songting alifariki mwaka 2001 katika mji wa Hangzhou kutokana na ugonjwa.


  [Burudani za Muziki]Maua ya orchis katika Majira ya Spring