Lu Rirong
中国国际广播电台

Bw. Lu Rirong alizaliwa tarehe 1 mwezi Juni mwaka 1933 katika wilaya ya Jun mkoani Hubei. Alishiriki kwenye maonesho ya sanaa mwaka 1945, mwaka 1950 akawa mpiga fidla na zeze la kichina. Baadaye alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha sanaa cha kaskazini magharibi, kujifunza zeze la kichina, utungaji muziki na uongozaji wa bendi. Mwaka 1954 alihitimu masomo na kuwa mwalimu katika chuo chake kufundisha upigaji wa zeze la kichina na uongozaji wa bendi. Sasa yeye ni mwalimu anayefundisha wanafunzi waliopata shahada ya pili katika chuo cha muziki cha Xian na kuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya muziki wa ala za jadi ya jumuiya ya wanamuziki ya China.

Katika uzoefu wa ufundishaji katika miaka karibu 50 iliyopita Lu Rirong alifanya shughuli mbalimbali za ufundishaji, upigaji ala za muziki, utungaji muziki na uongozaji wa bendi. Alitunga muziki wa aina zaidi ya 150 ya zeze la kichina, muziki wa ala moja zaidi ya 20, muziki wa ala nyingi zaidi ya 20 pamoja na makala ya kitaaluma zaidi ya 10.

Katika ufundishaji wake, Bw. Lu Rirong anaunganisha pamoja ufundishaji, upigaji wa ala za muziki, utungaji muziki na utafiti wa nadharia. Anataka wanafunzi wajiendeleze katika pande mbalimbali. Upigaji wa ala za muziki wake ni wa kupendeza, sauti ya muziki ni nyepesi, wazi na yenye hisia zake. Ustadi wake wa upigaji wa ala za muziki umeendelezwa kwenye msingi wa utamaduni wa muziki wa jadi na sehemu ya Shanxi. Mwaka 1960 katika semina iliyofanyika huko Shanghai kuhusu masomo ya upigaji wa zeze la kichina na gambusi alicheza muziki aliotunga “Muziki wa Mihu” na “Xintianyou” ambayo ilisifiwa na wataalamu kuwa ni uanzishaji wa mtindo na ustadi wa aina mpya.

Msingi wa utungaji muziki wake ni juu ya msingi wa muziki wa jadi wa huko ambao ni kama wenye harufu ya udongo wa uwanda wa juu. Muziki wa aina mbalimbali ya “Mtindo wa Muziki wa Shanxi”, “Mtindo wa Muziki wa Wanwan” ni ya mitindo tofauti kubwa ambayo inawaburudisha watu kwa mila na desturi ya wenyeji wa huko.

Umaalumu wake katika kuongoza bendi ni wenye uchangamfu mkubwa na mtiririko wa mfululizo. Muziki mzuri kadha wa kadha uliochezwa na bendi aliyofundisha kwa miaka mingi, ambayo ni bendi ya orchestra ya chuo cha muziki cha Xian, ilisifiwa sana na wanamuziki wa nchini na wa nchi za nje.

Makala alizoandika kuhusu nadharia ya muziki ni pamoja na “Umaalumu na Upigaji wa Muziki wa Zeze ya Mtindo wa Shanxi”, “Muziki wa Kale wa Changan unaendea Duniani kwa Mara ya Kwanza” na “Mchango wa Sanaa ya Uchezaji zeze ya Hua Yanjun kwa Ufundishaji wa Ustadi wa Zeze”.

Tokea miaka ya 80 alialikwa kufanya maonesho na kufundisha muziki katika nchi nyingi zikiwemo Japan, Ujerumani, Ufaransa na Singapore. Mwaka 1992 alitunukiwa sifa na baraza la serikali ya “mtaalamu aliyetoa mchango mkubwa wa China”.


  [Burudani za Muziki]Opera ya Meihu