Liu Dehai
中国国际广播电台

Bw. Liu Dehai ni mchezaji maarufu wa ala ya muziki ya gambusi ( lute ) na ni mmoja wa wachezaji hodari waliokomaa mwishoni mwa miaka ya 50 nchini China. Watu humwita kuwa ni bingwa mkubwa wa gambusi, na amejulikana nchini na katika nchi za nje.

Bw. Liu Dehai alizaliwa mkoani Shanghai mwaka 1937. Alipokuwa kijana katika shule ya sekondari alikuwa anapenda sana ala za muziki wa jadi na kuonesha kipaji chake. Mwaka 1950 alianza kujifunza uchezaji wa zeze na filimbi, na alishiriki katika shughuli za bendi ya ala za muziki za jadi ya Radio Shanghai baada ya masomo. Mwaka 1957 alishinda mtihani na kuandikishwa na chuo cha muziki cha taifa na kuanza kujifunza uchezaji wa gambusi.

Uchezaji wake wa gambusi ni wenye ustadi mkubwa, sauti ya gambusi aliyocheza inabadilika sana kutokana na muziki tofauti ambayo inawapa wasikilizaji kumbukumbu nyingi. Uchezaji wake ni kuunganisha ubora wa mabingwa wa sehemu mbalimbali na umeendeleza ustadi wa uchezaji wa gambusi.

Kutokana na msingi wa uchezaji wa jadi wa gambusi, Bw. Liu Dehai alifanya uvumbuzi na mageuzi katika uchezaji kutokana na maudhui ya muziki. Kwa mfano ili kuongeza kasi ya muziki anapocheza gambusi anatumia pia kidole gumba cha mkono wa kushoto ikilinganishwa na uchezaji wa jadi ambao kidole hicho hakitumiki katika uchezaji wa gambusi.

Muziki anaopiga Bw. Li Dehai ni wa aina mbalimbali kutoka muziki wa kale kama vile “Mtego” hadi muziki wa kisasa “Muziki wa Ngoma ya Kabila la Wayi”. Muziki anaopiga ni kama anawasimulia watu hadithi ambapo wasikilizaji wanajiona kama wako katika mazingira hayo.

Bw. Li Dehai anarekebisha nyimbo nyingi kuwa muziki wa gambusi ambazo ni pamoja na “Mto Liuyang”, “Wageni Kutoka Mbali Msiondoke” na “Dada Wawili wa Mbugani”.

Bw. Liu Dehai pia alitunga muziki kadhaa ukiwemo “Swain”, “Mzee Mtoto” na “Safari kwa Kwao”. Na amepata mafanikio katika kufanya uvumbuzi wa uchezaji wa gambusi na utungaji wa muziki. Tokea mwaka 1978 hadi mwaka 1981, Bw. Liu Dehai alifanya ushirikiano na bendi ya Marekani ya Boston Symphony Orchestra , bendi ya Symphony Orchestra ya Berlin ya magharibi.

Mafunzo makali, uzoefu wa miaka mingi wa kufanya maonesho ya muziki, ufundishaji wanafunzi pamoja na uzoefu wa kimaisha vimemfanya awe mwanamuziki mahiri. Hivi sasa yeye ni profesa katika chuo cha muziki cha taifa na ni mratibu wa kamati ya kudumu na naibu mkurugenzi wa kamati ya sanaa ya maonesho ya jumuiya ya wanamuziki ya China. Aliwahi kufanya maonesho na kufundisha katika nchi na sehemu zaidi ya 30 duniani na ametoa mchango mkubwa katika kuunganisha uchezaji wa gambusi na bendi ya Symphony Orchestra .



  [Burudani za Muziki]Kuvinjari kutoka Mafichoni