Liu Mingyuan
中国国际广播电台

Bw. Liu Mingyuan ni mmoja wa wachezaji hodari kabisa wa ala za muziki za jadi karibu nusu karne iliyopita na ni mchezaji wa ngazi ya juu kabisa katika majukwaa ya muziki ya China na nchi za nje. Bw. Liu Mingyuan ni hodari sana kucheza mazeze ya kichina yanayojulikana kwa “Banhu”, “Gaohu”, “Erhu”, “Zhonghu”, “Jinghu” na “Zhuihu”. Inasemekana kuwa hakuna mchezaji anayemzidi katika uchezaji wa “Banhu” na “Zhonghu” kwa hivi sasa.

Bw. Liu Mingyuan alizaliwa mjini Tianjin mwaka 1931, alianza kujifunza uchezaji wa “Banhu” na “Jinghu” kutoka kwa mama yake alipokuwa na umri wa miaka 6, na alipokuwa na umri wa miaka 11 alishiriki bendi za “Bailing” na “Minyue” na kujifunza muziki wa filimbi na zeze, na muziki wa Guangdong, opera ya Beijing na Opera ya Hebei. Kati ya mwaka 1947 na mwaka 1952 alikuwa mchezaji wa ala za muziki katika vikundi vya nyimbo na ngoma za “Shengli”, “Huanggong” na nyingi nyinginezo. Mwaka 1957 alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya muziki ya tamasha ya 6 ya kimataifa ya vijana.

Bw. Liu Mingyuan licha ya kucheza zeze la kichina, yeye pia ni hodari sana kucheza piano na aliwahi kuwa mchezaji wa piano katika muziki wa jazz. Aliwahi kujifunza nyimbo za kabila la wamongolia hivyo anafahamu fika mtindo wa muziki wa kimongolia.

Bw. Li Mingyuan ametoa mchango mkubwa katika mageuzi ya utengenezaji wa mazeze na ufundishaji muziki, alifanikiwa katika utengenezaji wa “Banhu” yenye sauti ya juu na “Zhonghu” yenye sauti ya kati. Toka miaka ya 50 alianza kufundisha wanafunzi na kuwa profesa wa uchezaji wa ala za muziki katika chuo cha muziki cha taifa. Alifariki dunia mwezi Februali mwaka 1996.



  [Burudani za Muziki]Mwaka wa Heri na Baraka