Fu Cong
中国国际广播电台

Bw. Fu Cong alizaliwa mjini Shanghai tarehe 10 mwezi Machi mwaka 1934 katika familia ya msanii na mwanaelimu, baba yake alikuwa msomi maarufu, mwana-nadharia wa sanaa na mtafsiri nchini China. Fi Chong alipokuwa na umri wa miaka mitatu au minne aliweza kuhisi mvuto wa muziki na kuonekana kupenda sana muziki. Alianza kujifunza kucheza piano kutoka kwa mwanamuziki wa Italia Bw. Mario Paci alipokuwa na umri wa miaka 7, na alijifunza uchezaji wa piano kutoka kwa bibi Ada Bronstein kutoka Urusi mwaka 1951.

Mwaka 1953 Bw. Fu Chong alishiriki mashindano ya piano akiwa mchezaji pekee wa China katika tamasha ya nne ya kimataifa ya vijana, na alipata tuzo ya ngazi ya tatu. Mwezi Machi mwaka 1955 mashidano ya kimataifa ya 5 ya Chopin yalifanyika mjini Warsaw. Bw. Fu Cong alichukua nafasi ya 3 kwa kupata pointi zinazokaribia sana na pointi za wachezaji waliochukua nafasi ya kwanza na ya pili miongoni mwa wachezaji 74 duniani.

Baada ya mashindano kumalizika, Bw. Fu Cong alibaki nchini Poland kujifunza upigaji wa piano hadi alipomaliza mafunzo mwishoni mwa mwaka 1958. Katika muda huo Bw. Fu Cong alirejea China kupumzika kati ya mwezi Agosti na Oktoba mwaka 1956, mjini Beijing akishirikiana na bendi ya symphony ya Shanghai alicheza muziki wa Mozart. Bw. Fu Cong aliondoka Poland mwezi Desemba mwaka 1958 na kuishi London, Uingereza.

Katika muda wa miaka 20 wa miaka ya 60 hadi 70, Bw. Fu Cong alifanya maonesho ya muziki kiasi cha 2,400; aliwahi kufanya ushirikiano na wanamuziki wengi wa kimataifa wakiwemo Bw. Menuhin, Bw. Barenboim na Bw. Chung Kyung-Wha; Alirekodi sahani za muziki kiasi cha 50; Aliwahi kuwa mwamuzi wa mashidano ya piano ya kimataifa ya Chopin na Elizabeth pamoja na mashindano ya piano yaliyofanyika nchini Norway, Italia, Uswisi, Ureno na nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki. Jarida la the Times lilimsifu kuwa ni “Mwanamuziki mkubwa kabisa wa China kwa hivi sasa”.

Mwaka 1976 Bw. Fu Cong alifanya maonesho ya muziki katika chuo cha muziki cha taifa. Baada ya hapo karibu kila mwaka alirejea China kufanya maonesho na ufundishaji mjini Beijing, Shanghai, Xian, Chengdu na Kunming. Licha ya kucheza muziki wa watungaji maarufu wa duniani alikuwa na ushirikiano na bendi ya taifa kucheza muziki wa Beethoven. Uzoefu wake katika mambo ya sanaa na moyo wake wa kufundisha wanafunzi umemfanya aheshimiwe sana na waalimu na wanafunzi wa muziki.



  [Burudani za Muziki]Muziki wa Usiku wa Chopin