Song Fei
中国国际广播电台

Bibi Song Fei (1969---) ni mchezaji maarufu wa zeze la “Erhu”, anafahamu uchezaji wa ala za muziki za aina 13, hivyo anasifiwa kuwa ni “malkia wa ala za muziki za jadi”.

Bibi Song Fei alipokuwa na umri wa miaka 7 alifundishwa na baba yake Bw. Song Guosheng ambaye alikuwa profesa wa chuo cha muziki cha Tianjin na ni bingwa wa Erhu. Mwaka 1987 alifaulu mtihani na kusoma katika chuo cha muziki cha taifa. Alihitimu masomo yake mwaka 1991 na kuwa mchezaji wa Erhu katika bendi ya ala za muziki za jadi ya taifa. Mwaka 1998 akiwa mwanafunzi wa shahada ya uzamili alijifunza uimbaji na uchezaji wa ala za muziki za Erhu na kinanda cha kale.

Tokea aliposoma katika shule ya sekondari bibi Song Fei alishiriki mara kwa mara kwenye mashindano ya ala za muziki za jadi nchini na alipata tuzo mara nyingi. Alitembelea sehemu nyingi duniani, hususan wakiwa mwakilishi wa wanamuziki wa China alicheza muziki wa kichina katika Golden Concert Hall ya Vienna.

Katika miaka ya 90 ya karne ya 20 bibi Song Fei akifuata bendi ya wanawake iliyoongozwa na bibi Zheng Xiaoying alifanya maonesho katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China. Licha ya hayo wao pia walifanya maonesho katika Ulaya. Safari moja aliongeza muziki mmoja kutokana na matakwa ya wasikilizaji, alipiga muziki wa Flight of the Bumble Bee kwa Erhu, alishangiliwa sana na wasikilizaji wa nchi za magharibi.

Mwaka 1996 bibi Song Fei akishirikiana na wanamuziki wengine 9 wa kike walianzisha bendi ndogo ya ala za muziki za jadi ili kuendeleza muziki wa jadi. Katika sikukuu za Spring za mwaka 1998 na 1999, bibi Song Fei akifuata bendi ya ala za muziki za jadi ya taifa alifanya maonesho mara mbili katika Golden Concert Hall, muziki wa Erhu aliocheza bibi Song Fei uliwasisimua wasikilizaji.

Mwaka 1999 bibi Song Fei alipofika kileleni katika uchezaji Erhu, ghafla alichagua kazi ya kufundisha, akisema kuwa anataka vijana wengi zaidi washiriki katika harakati za kuendeleza uchezaji wa ala za muziki za jadi. Mwaka 2002 bibi Song Fei alifanya maonesho ya uchezaji wa ala za muziki wa solo, alicheza aina 13 za ala za muziki na kufuatiliwa sana na wanamuziki wa nchini.

Muziki uliotungwa na bibi Song Fei na kupendwa na watu wengi ni pamoja na “Mwezi unaoonekana Kwenye Chemchem mbili”, “Milio ya ndege Kwenye Mlima” na “Muziki wa Ukuta Mkuu”.  [Burudani za Muziki]Kusikiliza Mvumo wa Misunobari