Muundo wa Utaratibu wa Umilikaji wa Vyombo Vya Uzalishaji Mali

中国国际广播电台


  

 

Kutokana na katiba ya China, katika kipindi cha mwanzo cha ujamaa, China ilishikilia utaratibu wa kimsingi wa uchumi ambao umilikaji wa vyombo vya uzalishaji mali wa umma ni uti wa mgongo na kuweko maendeleo ya pamoja ya umilikaji wa aina mbalimbali, kushikilia utaratibu wa ugawaji wa mapato ambao ugawaji wa mapato kutokana na kazi zilizofanyika ni njia kuu ya ugawaji wa mapato wa aina mbalimbali. Hivi sasa uchumi wa umilikaji nchini China ni pamoja na uchumi wa taifa, ushirika, binafsi, kujiajiri, ushirikiano, utaratibu wa hisa, uwekezaji wa wafanya biashara wa kigeni na wa Hong Kong, Macau na Taiwan.

Uchumi wa taifa ni aina ya uchumi ambayo serikali inamiliki vyombo vya uzalishaji mali; uchumi wa ushirika ni aina ya uchumi ambayo vyombo vya uzalishaji mali vinamilikiwa na mashirika ya umma; uchumi wa binafsi ni uchumi ambao watu binafsi wenye vyombo vya uzalishaji wanaajiri wafanyakazi, uchumi wa kujiajiri ni wa mtu kujitegemea kabisa katika uzalishaji kwa rasilimali na nguvu zeke mwenyewe. Uchumi wa ushirikiano ni aina ya uchumi ambayo shirika jipya la uchumi lililoungwa kwa uwekezaji wa viwanda au kampuni zenye umilikaji tofauti. Uchumi wa utaratibu wa hisa ni uchumi wa viwanda ua kampuni zilizoanzishwa na watu tofauti wenye hisa. Uchumi wa wafanya biashara wa kigeni ni uchumi ambao wafanya biashara wa kigeni kuanzisha viwanda nchini China kwa mujibu wa sheria au kanuni za sheria, ukiwa na mitindo ya aina tatu za kiwanda cha ubia kati ya China na mfanyabiashara wa kigeni, kiwanda kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya China na mfanyabiashara wa kigeni na kiwanda kilichowekezwa na mfanyabiashara wa kigeni peke yake. Uchumi wa uwekezaji wa wafanya biashara wa Hong Kong, Macao na Taiwan kuanzisha viwanda vyao China bara kwa mitindo ya aina tatu ya ubia, ushirikiano na mitaji ya wafanyabiashara wa huko peke yao kwa mujibu wa sheria au kanuni za sheria kuhusu nchi za nje za Jamhuri ya watu wa China.

Katiba ya China inapiga marufuku shirika au mtu yeyote kuhujumu au kuharibu mali za taifa au za ushirika kwa njia yoyote. China inalinda haki na maslahi halali ya uchumi usio wa umilikaji wa umma kama vile wa mtu aliyejiajiri au uchumi binafsi. Mali binafsi za raia hazishambuliwi.