Ujenzi wa Miundo Mbinu

中国国际广播电台


  

 

China ni nchi kubwa, barabara za China zinafika kila mahali nchini, zikiwemo barabara kuu 12 za ngazi ya taifa zenye umbali wa kilomita elfu 35 ambazo ni barabara 5 kutoka sehemu za kusini hadi sehemu za kaskazini na barabara 7 muhimu za kati ya sehemu za mashariki na magharibi, ambazo karibu zote ujenzi wake umekamilika.

Siku zote China inauchukulia ujenzi wa barabara kuwa ni jambo moja muhimu katika ujenzi wa miundo mbinu. Uwekazaji katika ujenzi wa barabara kati ya mwaka 1998 na mwaka 2001 ulikuwa Yuan bilioni 300 kwa mwaka. Barabara mpya zilifikia urefu wa kilomita elfu 67 zikiwa ni pamoja na kilomita 5,700 za barabara za kasi. Mwaka 2003, ujenzi wa barabara mpya zenye urefu wa kilomita elfu 36 ulikamilika. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, barabara za China zilifikia kilomita milioni 1 na laki 8, ikiwa ni pamoja na kilomita elfu 40 za barabara za kasi za kisasa. Aidha, serikali iliharakisha ujenzi wa barabara katika sehemu za kati na magharibi, ambazo zimeboresha mawasiliano ya sehemu hizo.

Ujenzi wa barabara kuu zote za China utakamilika mwaka 2008, ambapo miji ya Beijing, Shanghai, miji mikuu ya mikoa na miji mingine mikubwa zaidi ya 200 kwa jumla, itaunganishwa na barabara za kasi au barabara za ngazi ya juu.

RELI

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, urefu wa reli za China ulifikia kilomita elfu 73. Kati ya hizo zaidi ya kilomita elfu 20 ni zenye njia mbili pamoja na kilomita elfu 18 za treni ya umeme. Reli ya kwanza ya China inayovuka bahari kati ya mkoa wa Guangdong na mji wa Haikou ilianza kutumika tarehe 7 mwezi Januari mwaka 2003. Reli kati ya mikoa ya Qinghai na Tibet yenye umbali wa kilomita 1,142 ambayo inayojengwa kwenye uwanda wa juu kabisa duniani, ujenzi wake unatazamiwa kukamilika mwaka 2006. Hivi sasa China imekuwa moja ya nchi zenye shughuli nyingi za usafirishaji wa reli duniani, na pia ni nchi yenye ongezeko la kasi la usafirishaji wa reli na ufanisi mkubwa katika matumizi ya reli.

Tokea mwaka 1998, China iliinua kiwango cha reli ili kuongeza kasi za treni, hivi sasa treni nyingi za abiria zinasafiri wakati wa jioni na kufika stesheni ya mwisho wakati wa asubuhi ili kuwarahisishia abiria kufanya shughuli zao wakati wa mchana.

BANDARI

Ujenzi wa bandari za pwani ya China unafuata zilipo rasilimali za makaa ya mawe, makontena, na mawe ya madini ya chuma yanayoagizwa kutoka nchi za nje, njia za usafiri wa meli zenye kina kirefu za kuingia baharini, hususan kutilia mkazo ujenzi wa mfumo wa usafirishaji wa makontena. Serikali imejenga magati yenye kina kirefu kwa ajiri ya usafirishaji wa makontena katika miji ya Dalian, Tianjin, Qingdao, Shanghai, Ningbo, Xiamen na Xhenzhen, ambayo yameweka msingi kwa uundaji wa mfumo muhimu wa uchukuzi wa makontena, wakati baadhi ya magati ya kupakulia mafuta asili ya petroli na mawe ya madini ya chuma yaliyoagizwa kutoka nchi za nje, yalirekebishwa na kupanuliwa.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, bandari muhimu zilizoko kwenye pwani ya China, zimekuwa na mahali pa meli 1800, zikiwemo meli zaidi ya 530 zenye uwezo wa kubeba mizigo zaidi ya elfu 10. Bandari hizo zina uwezo wa kushughulikia tani bilioni 1.7 za mizigo kwa mwaka. Baadhi ya bandari kubwa zimekuwa na uwezo wa kushughulikia mizigo zaidi ya tani milioni, wakati bandari nane kubwa za Shanghai, Shenzhen, Qingdao, Tianjin, Guangzhou, Xiamen, Ningbo na Dalian ni miongoni mwa bandari 50 zinazoongoza kwa upakiaji na upakuaji wa makontena duniani.

USAFIRI WA NDEGE

Safari za ndege za China zinafika mabara yote ya dunia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, kulikuwa na viwanja vya ndege za abiria zaidi ya 140 vikiwa na safari zaidi ya 1000, ambazo ni pamoja na safari zaidi ya 160 zinazofika miji zaidi ya 60 ya nchi zaidi ya 30.

SIMU

Mwaka 2003, ongezeko la idadi ya simu mpya za nyumbani lilifikia milioni 49.08, na idadi ya jumla ya simu za nyumbani mwishoni mwa mwaka huo ilikuwa ni zaidi ya milioni 260. Kati ya hizo za mijini zilikuwa ni zaidi ya milioni 170 na za vijijini zilikuwa milioni 92.13. China ilianzisha utoaji wa huduma za simu za mikononi mwaka 1987, ambao ulikuwa na maendeleo ya kasi baada ya mwaka 1990, na ongezeko la wateja wapya lilikuwa ni zaidi 100%. Mwaka 2003, mtandao wa simu za mikononi ulifika katika miji yote mikubwa na wastani pamoja na miji midogo na ya wilaya zaidi ya 2,000. Ongezeko la wateja wapya lilifikia milioni 270, na jumla ya idadi ya wateja wa simu za mikononi ilikuwa ni zaidi milioni 530, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 110 kuliko mwaka 2002, ambapo watu 42 kati ya watu 100 walikuwa na simu za mikononi.